GET /api/v0.1/hansard/entries/1443067/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443067,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443067/?format=api",
"text_counter": 74,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mambo ambayo yalifanyika hapa ni ya kuhuzunisha. Watoto wetu wa kiume wakifa, wasichana wetu wataolewa na nani? Vijana wetu wanajimaliza au kumalizwa na dawa za kulevya na vitu vingine. Itakuwaje kukitokea vita kati ya Kenya na nchi nyingine? Huenda Kenya ikashindwa kwenye vita. Tunahitaji maombi. Tunafaa kuanza harakati za kufanya maelewano au dialogue . Hii inafaa kuhusisha watu wote kwa sababu hakuna mtu asiyemjua Mungu. Tunafaa kuketi pamoja ili tusemezane. Tunafaa kutafuta mbinu za kusaidia vijana wetu. Kuna suala la kuoa. Jambo la pili ni ukosefu wa kazi. Mhe. Rais pamoja na watu wengine wamekubali kuketi chini na vijana wetu. Mhe. Rais alisema kuwa yuko tayari kusikiza watu. Kwa hivyo, nawaomba Gen Z. Msikubali kwenda barabarani tena. Kilio chenu kimesikika mbinguni na duniani, hasa hapa Kenya. Jambo lingine ni kujua jinsi Gen Z watakavyopata kazi. Tumesema mambo mengi sana katika Seneti hii. Hata hivyo, hatujatoa suluhisho kwa mambo mengi. Wengine wamesema kuwa watu wafutwe kazi. Siungi mkono mapendekezo hayo. Unaweza kufuta mtu kazi na ukibaki na watano lakini bado utabaki na watu wabaya. Tunasoma katika Bibilia kuwa walikuweko watu watu wabaya kama Judas Iscariot. Aliharibu mambo mengi mpaka akaleta shida ulimwenguni. Kila eneo bunge hupata mgao wa the National Government-Constituencies Development Fund (NC-CDF). Pesa hizi ni nyingi. Kuna vijana wanaotaka kufanya kazi mashinani kama vile ujenzi lakini hawana pesa zinazohitajika. Wabunge wote wanafaa kuhakikisha kuwa sheria inafuatwa kuhusu NC-CDF. Sheria hiyo husema kuwa asilimia 30 za kazi zinafaa kupewa vijana ambao ni Gen Z, walemavu na wanawake. Wengi wa wabunge hawajakuwa wakifanya hivyo. Sheria hii inapaswa kuzingatiwa kwa makini ili Gen Z wapata nafasi za kazi mashinani. Kuna njia nyingine ya kusaidia vijana wetu. Tuna kaunti 47 ambapo kila mojawapo ina wizara karibu 10. Naomba magavana wote waangalie jinsi wamekuwa wakifanya kazi. Kuna watu wanaozembea kazini na wanaoiba pesa. Watu kama hao wapelekwe kortini na wale wengine wafutwe kazi ili vijana wetu wapate kazi. Vijana wetu ni washupavu na wanaelewa jinsi ya kufanya kazi. Vile vile tunaweza kutafuta nafasi za kazi katika Serikali ya Kitaifa. Mhe. Rais amekubali kunyenyekea. Kuna the National Employment Authority (NEA). Tunaomba aendelee kutilia mkazo ili vijana wetu wapate kazi. Mimi ni mwanakamati wa Kamati ya Leba na Ustawi wa Jamii. Miaka miwili iliyopita, vijana wetu walikuwa na shida nyingi. Wakati huu Serikali yetu ina idara inayotilia maanani mambo ya vijana wetu. Hili ni ombi langu kwa Mhe. Rais asaidie vijana wetu kupata pasipoti. Vijana wengi hawana pasipoti na vitambulisho kwa sababu ya kukosa pesa. Tunaweza kutenga kiasi fulani cha pesa za NG-CDF ili vijana wetu waweze kupata pasipoti na kugharamia mahitaji mengine kama vile kupimwa hali zao za afya kabla ya kwenda kule nje. Tunafaa kutafutia vijana wetu kazi. Tuna Wizara 21 za Serikali. Uchunguzi ufanywe ili kujua ni nani wameajiriwa katika wizara hizi. Iwapo kuna mtu ambaye amezembea kazini, anafaa kutimuliwa. Wale ambao wamepora mali ya umma wapelekwe kortini ili kuwe na nafasi za kazi kwa Gen Z. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}