GET /api/v0.1/hansard/entries/1443068/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443068,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443068/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninataka kusema ukweli. Huwezi kusafisha kikombe ndani ilhali nje ni kichafu. Hapa tuko Maseneta 67. Hatufai kuwanyoshea kidole Wabunge wa Bunge la Kitaifa, Mawaziri, Mhe. Rais au Mhe. Naibu wa Rais. Ningeomba tuanzie katika Seneti ya Kenya ambayo iko na Maseneta 67 na Kaunti 47. Tulipochaguliwa kama Maseneta, tuliletwa hapa tuangalie kazi za kaunti. Tuna kamati zaidi ya kumi katika Bunge hili la Seneti. Baadhi ya kamati hizo zina wanachama tisa. Ni jambo la aibu kuwa wanachama wengine hawajawahi kuonekana katika kamati zao. Unafaa ujiulize uliletwa hapa kufanya nini. Gen Z nawajulisha ya kwamba Maseneta wote wanafaa kuwa kazi Jumanne, Jumatano na Alhamisi. Ulizeni hao Maseneta hufanya kazi kivipi. Ni lazima tuanzie hapa kuangalia kaunti zinafanya kazi vipi kabla ya kuwanyoshea kidole watu wengine. Katika Bunge la Kitaifa, Wabunge wengi huhudhuria viko wakati wa kupiga kura tu. Inafaa muwaulize hao watu huwa wanafanya kazi gani. Tukimuweka Mungu mbele, mambo ya Kenya yataenda mbele. Uchumi wetu utakuwa sawa na nafasi za kazi zitapatikana katika serikali za kaunti na national Government. Tutalipa madeni na Serikali ya Kenya itakaa vizuri kwa kipindi hiki. Kwa hivyo, tuungane pamoja na tusiwe watu wa kunyosheana vidole bali tusemezane. Bw. Spika, nikimalizia, nakumbusha Serikali ya Kenya Kwanza na wale wengine wote katika Kenya mzima kwamba, kutimua CSs na Principal Secretaries (PSs) haitasaidia. Kitu cha kwanza ni kuangalia yule mtu ambaye hafanyi kazi ndio atimuliwe. Tunaweza wacha watu wawili na kama hawataangaliwa, basi hakuna kazi watafanya. Nakumbusha watu wa Kenya tena kwamba wakati watoto wa Israeli walitoka Misri, walifika mahali na wakaanza kupigana hadi Nabii Isaya alipowaambia, “njooni nyote tusemezane.” Huu ni wakati wa Kenya kusemezana. Makanisa, Senate, Gen Z na groups zote tuungane pamoja kama watu wa Kenya ili tuweze kusaidiana. Nawaambia Gen Z kwamba Kenya ni yetu sisi sote; wazee kwa vijana. Sisi kulingana na miaka yetu, tunaondoka. Tunataka mtushikilie na mfanye kazi kwa bidi ili uchumi wa kaunti zetu na Kenya nzima uimarike. Kwa mambo ya agriculture, CS afanye kazi pamoja na departments zingine kama vile trade na cooperatives . Pia kaunti governments zichimbe mabwawa ya maji ili wazee wasiende mbali kutafuta maji ya mashamba yao. Gen Z ambao wako na fikira za kulima pia waweze kulima wakitumia maji hayo. Wapewe pesa kutoka cooperatives. Department ya trade itafute soko kule nchi za ng’ambo. Nawahakikishia Gen Z kwamba kilio chenu kimesikika kwa Mungu na Kenya. Mambo haya yakifanyika vizuri, economy ya kaunti zetu zote 47 na Kenya nzima itaimarika na Kenya kama taifa itasimama imara. Bw. Spika, nikiwa Seneta wa Embu Kaunti, naunga mkono haya mazungumzo ili tuweze kutembea pamoja. Ni mimi wenu Seneta wa Embu Kaunti, Daktari Alexander Munyi Mundigi. Pia mimi ni Deputy Party Leader wa Democratic Party katika Serikali ya Kenya Kwanza. Naunga mkono."
}