GET /api/v0.1/hansard/entries/1443144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443144,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443144/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa hii fursa umenipa ili kuchangia huu mchakato wa kutathmini hali halisi ya nchi hii yetu ya Kenya. Kwanza kabisa, namshukuru Kiongozi wa Walio Wengi, Seneta wa Kericho, Sen. Aaron Cheruiyot na Kiongozi wa Walio Wachache, Seneta wa Kilifi, Hakimu Mstaafu, Sen. Steward Madzayo, kwa kuleta Hoja hii ya kuangalia hali halisi ya Kenya. Jambo la pili, nawashukuru Masenta kwa kukubali kubakia ili kuangalia vile Kenya ilivyo kwa sababu saa hii, Kenya iko katika njia panda. Bunge la Kitaifa liliamua kukimbia na kwenda nyumbani wakati Kenya inawahitaji. Nachukua hii fursa kwa niaba yangu na wananchi wa Taita-Taveta kutoa risala za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walipoteza watu wao wakati wa maandamano. Haya maandamano yalikuwa ni ya kupinga Mswada wa Fedha na yaliongozwa na vijana wanaojiita Gen Z ama kizazi cha zuma. Kwa hekima ya Mhe. Rais, aliona kwamba auondoe huo Mswada na urudi kwa Bunge la Kitaifa. Kwa sababu tuko mahali ambapo hatuaminiani, hekima nyingine ni vyema Bunge la Kitaifa, lirudi na liangalie mapendekezo ya Mhe. Rais ili tuwe na uhakika ya kwamba huo Mswada umeondolewa kikamilifu. Hii ni kwa sababu sheria inasema ya kwamba, baada ya siku 14, hata kama Mhe. Rais hajatia saini, basi ule Mswada utaanza kutekelezwa. Bi. Spka wa Muda, wakati tumekuwa katika njia panda, wakati mwingi kama Wakenya tumesimama na kuongea. Hii sio mara ya kwanza ambayo tumeanza kuongea kwa sababu ya nchi yetu. Mwaka wa 1997 tuliongea katika ule Ufungamano Inititative na mwaka wa 2019 pia tuliongea na kuja na mapendekezo yaliyoitwa Building Bridges Initiative (BBI), ingawaje ilienda vile ilienda. Sasa hivi pia, tukiona watu wanaandamana, hiki ni kiini tu cha juu ya kwamba Wakenya hawana furaha na yale yanayoendelea katika nchi yao. Ukiangalia, watafiti wengi ambao wanafanya utafiti Kenya, tayari washasema kwamba Wakenya hawana imani na uongozi na hawafurahii pale Kenya inapoelekea. Hawa vijana wa Kizazi cha Zuma walipigana na kuandamana kwa sababu ya huu Mswada wa Fedha lakini, hio sio shida pekee yake. Hicho kilikuwa ni chanzo tu---"
}