GET /api/v0.1/hansard/entries/1443148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443148,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443148/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Fedha na kufanya maandamano. Watu wakazinduka wakasema ni vyema tukae chini, tuongee na tuangalie kwa kina kwa sababu kuna shida nchini Kenya. Jambo la kwanza katika mchango wangu ni kuwa kila mtu afanye kazi yake. Tuko na Katiba ambayo imetupatia majukumu katika Serikali na iko na miguu mitatu. Mguu wa kwanza ni watendakazi ama Executive . Wa pili ni Bunge na wa tatu ni mahakama. Ukiangalia kwa sasa, hujui tofauti ya watendakazi ama Executive na Bunge kwa sababu Bunge limemezwa na Executive . Bunge haifanyi kazi yake ya uangalizi, kutunga sheria na uwakilishi. Kama Bunge ingekuwa inafaya kazi yake na wao ni wawakilishi wa wananchi, basi Mswada wa Fedha haungepita vile ulipita, ukapelekea maandamano na watu zaidi ya 40 kupoteza maisha yao. Wabunge wa Bunge la Kitaifa, wamekuwa kama watendakazi kwa sasa. Saa hizi wako na NG-CDF. Kazi yao ni kusema kwamba wamejenga manyumba, wamenunulia shule fulani basi na wamepea wazazi NG-CDF. Halafu, wanapiga mapicha na wanasema wamefanya kazi. Hio sio kazi ya Bunge; hiyo ni kazi ya watendakazi ama Executive. Wabunge wameacha kazi yao na huwezi kutofautisha kati ya Bunge na Executive. Bi spika wa Muda, kwa sasa, kazi za Executive zinafanywa na Wabunge. Utasikia Mbunge yuko na shilingi 160 milioni ya NG-CDF, amepewa pesa ya stima au ya barabara na hao Wabunge ni wakandarasi wao wenyewe. Kazi ya Mbunge ni kuangalia kama mkandarasi afanye kazi yake vizuri. Kama ni barabara imejengwa, imejengwa namna gani. Swali langu la kila siku ni kuwa kama ni wewe umetafuta mkandarasi na ameweka"
}