GET /api/v0.1/hansard/entries/1443150/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443150,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443150/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "kwa barabara vibaya, utamuuliza namna gani na ni wewe mwenyewe ambaye ulimtafuta mkandarasi wako mwenyewe na unapokea asilimia 10? Vile Mhe. Kajwang’ amesema, kuna ukabila katika uajiri wa wafanyakazi. Juzi, watu walikuwa wanaajiriwa katika Kenya Revenue Authority (KRA). Kati ya watu 600 ambao walifanyiwa interview ama mahojiano, watu 500 wanatoka katika kabila mbili. Kama Bunge ingefanya kazi yake vizuri, basi wangeweza kutegua hicho kitendawili cha ukabila katika Public Service. Ukiangalia katika kaunti zetu, zaidi ya asilimia 10 ya pesa ambayo inaenda kwa serikali za kaunti zinaibiwa. Hii ni kwa sababu wale Wabunge wa kaunti wanafanya kazi kana kwamba wao ni watendakazi. Wanatoa zabuni kwa wanakandarasi wao. Kazi inafaywa ambayo haifai ama shoddy job kwa kizungu, na hawawezi uliza maanake wale wakandarasi ni wao. Kila mtu angefanya kazi yake, basi hawa vijana wetu hawangelalamika wakisema kwamba wamefinyika na uchumi wetu umeharibika. Wale waliozungumza hapa wamesema kwamba kuna asilimia 30 ambayo imetengwa kwa vijana, kina mama na walemavu. Kama Mbunge na MCA atafanya kandarasi zake mwenyewe, je, wale kina mama, vijana na walemavu watapata lini nafasi ya kufanya kandarasi na kujitengenezea pesa? Kwa hivyo, kama kila mtu angefanya kazi yake mwenyewe, basi Kenya yetu ingekuwa nzuri. Ufisadi umekidhiri. Magavana na mawaziri wanaitwa katika Bunge la Senate ama la Kitaifa na wanakimbia mahakamani. Mfano mzuri ni Gavana wa Isiolo. Ameitwa kwa Seneti akakimbia mahakamani kusimamisha kuitwa kwake. Sasa huyu Gavana atawajibika namna gani na atasema ametumia pesa namna gani? Mahakama wangesema tu, enda kwa Seneti, hatutakupatia order zozote za kutoenda huko, Kenya ingekuwa nzuri. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}