GET /api/v0.1/hansard/entries/1443151/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443151,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443151/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Sheria inasema kwamba mtu ambaye amekataa kuja Bunge, Inspekta wa Polisi amshike, ikiwa ni gavana au waziri, aje Bunge. Ila Inspekta Mkuu wetu wa polisi ameshindwa kuwaleta wafisadi katika Bunge letu. Sasa ikiwa kila mtu hafanyi kazi yake, inaonyesha kwamba ufisadi utakithiri na hatutapata maendeleo. Hao watu wanaoitwa Gen Z hawatawacha kupigania haki zao. Bi. Spika wa Muda, ningependa kusema kwamba vijana walifanya maandamano na ni haki yao kulingana na Ibara ya 37. Walifanya maandamano ya amani ila wakora waliingia na kuharibu. Naona wengine wao waliletwa na Serikali ili kuonyesha kwamba wale waandamanaji hawajui wanachofanya. Jambo la pili ningependa kulisema ni kulingana na Ibara ya Kwanza. Inasema kwamba nguvu za uongozi zinatoka kwa mwananchi. Zile nguvu anaweza kuzitekeleza mwenyewe moja kwa moja au kupitia yule aliyemchagua. Kama nguvu za uongozi zinatoka kwa mwananchi, basi itakuwaje mwananchi asikizwi anavyosema? Tumekuwa na gharama. Mwaka uliopita, kulikuwa na Mswada wa Fedha ambao ulileta Housing Levy na tax nyingi sana. Wakati wa kupigania uhuru, tulipigania kwa sababu tatu. Ya kwanza ni kutozwa ushuru kupita kiasi. Ya pili ilikuwa mambo ya mashamba na ya tatu ni slavery . Sasa hivi pia watu wameona wametozwa ushuru sana na hawana njia ya kujikwamua. Wanapigania uhuru wa tatu. Kwa hivyo, kama tungekubali kwamba nguvu za uongozi ziko kwa mwananchi na sisi tumechaguliwa na kukopeshwa zile njia, basi Mhe. Rais angesikiliza vile wananchi wanasema. Sisi Wabunge tungesikiliza wananchi wanavyosema kwamba hatutaki huo Mswada wa Fedha kwa sababu inatufinya. Unatuibia pesa kwa kuchukua kutoka mifuko yetu. Bi Spika wa Muda, katika Chuo Kikuu cha Harvard, wasomi walikuja na nadharia inaoitwa principal agent theorem . Katika ile nadharia ambayo inatumika kwa mambo ya kiuchumi na tutaitumia pia kwa mambo ya uongozi. Walisema kwamba katika uongozi, mkuu ni mwananchi, kisha mjumbe ni yule amechaguliwa. Kwa hivyo, haiwezekani kwamba wewe mjumbe umechaguliwa kama Mbunge, Seneta, Mhe. Rais au gavana unajiamulia mambo yako mwenyewe bila kuhusisha mwananchi. Mwananchi akitoa sauti yake unamuuliza, unasema nipige ‘la’ kwa Mswada, uliisoma? Mwananchi akisema piga ‘la’ kwa huu Mswada kwa sababu unanifinya na wewe ni mjumbe wala sio mkuu, tusikize. Tulisikia kwamba kuna Wabunge waliohongwa kwa shilingi 2 milioni. Unahongwa kwa shilingi 2 milioni kutopigia Mswada vile mwananchi wako anataka? Katika hii nadharia ya mkuu na mjumbe, huko ni kukosa heshima na ni dharau na kuonyesha kiburi kwa aliyekuchagua. Mwananchi aliyekuchagua lazima aje mbele na wewe na mapenzi yako na matumbo yako yaje nyuma. Tuwe na heshima na tujue kuwa mwananchi yuko mbele na ndiye mwajiri wetu. Sisi tunaitwa wajumbe kwa sababu wewe sio mkuu. Nguvu za uongozi ziko na wananchi. Wakati tumesimama kuwa na kiburi kwa sababu tumepata pesa kidogo na kuonyesha kwamba ni wewe unayekalia mwananchi, atafanya tulivyoonyesha katika hiki kizazi cha Gen Z. Bi. Spika wa Muda, Wabunge wamepewa kazi ya kutengeneza Bajeti. Nilikuwa nazungumza na Mbunge wangu ambaye yuko kwa Kamati ya Bajeti. Anasema Treasury The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}