GET /api/v0.1/hansard/entries/1443152/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443152,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443152/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "wanaleta bajeti katika Bunge ila hakuna njia ya kubadilisha bajeti kwa sababu Treasury na Serikali imeleta ile bajeti. Ikiwa kazi ya Bunge ni kutunga bajeti, kwa nini hakuna ugavi wa kisawa sawa ya rasilimali za nchi? Maeneo mengine kama Taita-Taveta yameachwa nyuma sana. Hakuna miradi tunayopata zaidi ya shilingi 500 milioni au shilingi 1 bilioni. Tuko na barabara ya Bura- Mgange na Wundanyi-Mtomogoti. Hiyo barabara ilianza mwaka wa 2020 na hadi leo imewekewa kama shilingi 200 milioni pekee. Tumepitisha bajeti nne ya zaidi ya shilingi 3 trilioni na tunakosa shilingi 2 bilioni pekee kumaliza zile barabara. Hii ni kwa sababu gani? Hatuna Mhe. Rais na kura zenu ni chache. Tusipoyangalia haya mambo, maeneo mengi wanakosa maendeleo kwa sababu hawawezi kuwa na Mhe. Rais na hawako karibu nae. Kuwekewa pesa ya maendeleo inakuwa shida sana. Ni jukumu la Serikali na Bunge kuangalia kwamba ugavi wa rasilimali uwe sawa. Bi. Spika wa Muda, kwa sababu Mswada wa Finance haukupita, basi Division of Revenue Act (DORA) itarudi na Comission on Revenue Allocation (CRA) pia itabadilika. Naomba Maseneta wenzangu kwamba ule Mswada wa DORA ukirudi, tusijaribu kupunguza pesa yetu iwe chini ya shilingi 400.1 bilioni tulivyopitisha kwa DORA. Ni kwa sababu gani? Pesa zinazooenda kwa magatuzi ni chache muno. Afya na kilimo ambayo ni muhimu sana imegatuliwa ilhali pesa ambayo tunapeleka kule ni finyu sana. Kwa hivyo, nitashangaa mradi ikirudi hapa na tuseme tunapunguza pesa za magatuzi ilhali tumeona kiburi na majivuno ya wale watu wanaofanya kazi katika Serikali ya Kitaifa ambao wananunua saa ya mkono ya shilingi 3 milioni, viatu vya shilingi 500,000 na magari ya kifahari kama vile Lexus ilhali wengi wao walikuwa maskini tukiwa hapa nao kama Maseneta. Sisi kama watu waofanya kazi ya kulinda magatuzi, kama nilivyosema katika mada yangu, tutakuwa tumeshindwa kutekeleza majukumu yetu kama Maseneta kama tutakubali pesa ipungue chini ya shilingi 400.1 bilioni. Jambo la mwisho ni kuhusu taasisi ambaza zimepewa jukumu ya kuangalia mambo ya ufisadi, ikiwamo DCI na EACC. Ikiwezekena EACC itupiliwe mbali kwa sababu hakuna kazi wanayoifanya. Kuna watu pale kwetu walishikwa na sakata ya pilau. Kwamba walinunua pilau ya shilingi milioni mbili. Tulipofuatilia tulipata kwamba hawakununua kwenye hiyo hoteli. Tumepeleka sakata hiyo kwa DCI na EACC, hakuna hatua ilichukuliwa dhidi ya watu hao. Wanatembea kila mahali wakijigamba kuwa hawajapelekwa mahali. Nilienda kwa DCI nikaambiwa niwe witness, nisimame katika mahakama. Tume ya EACC wameshindwa kufanya kazi yao kwa sababu wao pia ni wafisadi. Haiwezekani kupeleka mbuzi kwa mahakama ya fisi. Maseneta wengi wamezunguza juu ya hili suala la kuongezwa mshahara ya Wabunge. Tumekataa huo mshahara. Huo mshahara na zile pesa zitakazokusanywa tukipigana na ufisadi, walimu wa JSS na clinical officers wataajiriwa. Itawezekanaje kuna shida kule kwa watoto wa JSS ya kufunzwa na walimu wawili ama watatu halafu tuambiwe ya kwamba tunaongezewa pesa? Hizo pesa tumezikataa. Zipelekwe kuajiri walimu wa JSS Ninauliza hili kwa sababu nilikuwa katika taaluma ya ualimu miaka iliyopita. Kama"
}