GET /api/v0.1/hansard/entries/1443156/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443156,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443156/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante. Curriculum y etu iko spiral. Ukifunzwa kitu kimoja leo, inafuatilia baada ya miaka miwili unaipata huko mbele inajengwa. Kama leo hii haujafunzwa vizuri, je, ukienda huko mbele, utaelewa masomo? Kwa hivyo, katika huu mtaala wa JSS, watoto wetu hawafundishwi vizuri. Hivyo basi, tunamaliza kizazi chote kwa sababu ya kukataa kuajiri walimu. Vile vile, Serikali ilisema ya kwamba ikifikia Septemba, itaajiri walimu wote 46,000 ambao wako katika kandarasi. Serikali itafute pesa na iajiri hawa walimu ili watoto wetu wapate elimu iliyo bora na si bora elimu. Kwa hayo mengi, ninaunga mkono Hoja hii. Asante Bi. Spika wa Muda."
}