GET /api/v0.1/hansard/entries/1443338/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443338,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443338/?format=api",
"text_counter": 108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii nami nitoe kauli yangu. Kwanza, nitoe rambi rambi zangu za pole kwa wale vijana waliopoteza maisha yao katika haya maandamano. Pia, niseme pole kwa wale ambao wanaugua mahospitalini. Tunawaombea afueni na warudi kwenye shughuli zao. Nchi yetu inashida tatu. Hizo shida tatu ndizo zinasababisha hii nchi kutotawalika au kuwa na misukosuko. Shida ya kwanza ni ukabila, ya pili ni ufisadi na ya tatu ni ukosefu wa usawa. Hawa Gen Z wamekuja kutuondolea haya mambo matatu kutuonyesha kwamba ikiwa tutaendelea na haya mambo matatu, hapana mahali tutaenda. Wametuonyesha kwamba wao hawana ufisadi wala ukabila. Wanataka usawa. Ikiwa tutafuata hii filosofia ya hawa Gen Z, bila shaka tutaleta mabadiliko katika nchi yetu na itaweza kutawalika. Bw. Naibu wa Spika, vijana hawa wamesoma, hawana balaa. Ni wale waliopata elimu ya bure, iloyokuwa ya maana na maradufu wakati wa Mhe. Kibaki akiwa na msaidizi wake Mhe. Kalonzo Musyoka. Tunachoomba ni hao vijana wasichukuliwe nguvu na polisi ila washirikiane nao. Pia, waachwe wafanye mambo yao kwa sababu ni vijana walionyesha umahiri na kwamba wanayo nia nzuri ya kubadilisha hii nchi. Hawana nia mbaya, wala hawataki fujo. Sijasema kwamba tuchukuwe filosofia yao kwa uharibifu wala kwa fujo. Filosofia iwe ya kuondoa yale mambo matatu ambayo nimetaja. Hawa vijana wametokea sio kwa sababu ya Finance Bill ila kwa sababu tofauti tofauti ambazo zinawakwaza katika maeneo yao wanapoishi. Kwenye sababu nyingi zinazowakwaza nitataja chache. Ni kwa sababu ya ongezeko ya school fees . Wengi hawasomi, wamefukuzwa manyumbani wana randararanda. Mambo ya university, umeme, housing levy na ushuru umeongezeka mara dufu. Vijana hawa kwa mara nyingi hawana njia ya kujihami kwa vyovyote. Vile vile, ukichunguza vijana kama hawa utapata kwamba wanaona ukosefu wa usawa kwa mfano wa makazi. Utaenda ofisi ukute kazi kuanzia juu hadi chini ni kabila moja au mbili ilhali Kenya tuko na makabila zaidi ya arobaini. Kule Lamu Port, kuna vijana wetu mia moja waliochukuliwa miaka minne iliyopita wakiwa kama casuals. Hadi wa leo ni vibarua, hawajawahi kuandikwa"
}