GET /api/v0.1/hansard/entries/1443347/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443347,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443347/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "kutoka kwa wakubwa wao na kuambiwa kwamba isipoenda hivyo ni wao wataumia. Wakishachukuwa zile order maneno yanabadilika kukichafuka, inakuwa wao ni sacrificial lamb . Kwa hivyo, hii ufisadi---- Hata hapa Bunge wabunge wanaitwa kwenye Parliamentary Group (PG), kuambiwa lazima huu Mswada mpitishe. Kwa nini mbunge akubali kusema nimepewa milioni mbili kupitisha huu Mswada? Kwa nini Rais atoe milioni mbili ahonge mbunge akijua kuwa huo Mswada ni mzuri? Hayo yote ni ufisadi kutoka juu hadi chini. Ukipeleka kesi Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) unaulizwa unamjuwa nani au huyu unayemleta kwa hii kesi anamjuwa nani. Niko na Ushahidi. Nilipokuwa mwenyekiti wa Child Welfare Society of Kenya, nilipata organization hiyo ikiwa na ufisadi hali ya juu. Nilipo peleka kesi EACC pamoja na ushahidi, waliniuliza huyu mama ako connected na nani kabla hawajamguza. Kwa hivyo, haya mambo ya ufisadi yanaanzishwa huko juu yakielekea chini. Sio kitu ambacho ni ofisa au mtu mdogo ameamua kufanya yale mambo ila anapewa order. Hata hao wabunge wakipitisha ile kitu walipewa order na Rais kwamba huu Mswada lazima upite na wakahongwa . Kama ni kusema ukweli, ukweli usemwe na mambo yajulikane wazi. Ikiwa ufisadi utaendelea na ikiwa Rais hatajaribu kungángána na ufisadi -maanake yeye ndiye fisadi mkubwa - basi hakuna mahali tutaenda. Wale ambao ni fisadi Rais amejitokeza kimasomaso kuwalinda. Ina maana hajaamua kupigana na ufisadi kama Rais wa nchi. Tunataka Rais apambane na ikiwa hawezi atoe nafasi wanaume wachukue nafasi hiyo wafanye kazi. Tunataka mabadiliko na tumeletewa na vijana. Wasirudi nyuma, tunawaunga mkono, tuko nao. Hao vijana waendelee vivyo hivyo. Wameonyesha umahiri na ungwana kwamba hawana haja na mali ya mtu, kuiba wala kuharibu. Wao wanataka haki yao na lazima ipatikane. Bw. Naibu wa Spika, nikimalizia kwa kuwa mimi sio mtu wa maneno mengi, nawaambia vijana wachukuwe kura kwa wingi. Hiyo ndiyo silaha ya kupambana na adui. Asanteni sana, nimeshukuru. Naunga mkono."
}