GET /api/v0.1/hansard/entries/1443372/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443372,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443372/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi pia niweze kujumuika pamoja na Senators wenzangu kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge hili na pia ukaungwa mkono na Kiongozi wa Walio Wachache. Naungana pamoja na Wakenya na viongozi wenzangu kutoa risala za rambi rambi kwa familia za vijana wetu ambao walipoteza maisha yao wakati ambapo walikuwa wamejitokeza kupigania haki yao katika sehemu mbali mbali za Jamhuri yetu. Vijana hawa ambao wamepoteza maisha yao walikuwa na umri mdogo sana. Walikuwa wanaelekea katika umri ambao wanaweza kutegemewa katika jamii. Lakini, kwa sasa, wamepoteza maisha yao. Kwa hivyo, ni jambo la huzuni sana sisi kama viongozi katika taifa hili la Kenya kuona kwamba hawa vijana wamepoteza maisha wakati wa uongozi wetu. Natoa rambi rambi zangu na kusema pole kwa wazazi ambao wamepoteza wapendwa wao kwa sababu ya jambo hili la uchungu mkubwa. Bw. Naibu Spika, hawa vijana wa Gen Z walijitokeza katika kupigania mambo ambayo wanafaa wasikizwe. Kikatiba, hawa vijana wako na haki ya kupigania haki zao mahali ambapo wanaona hapaendi vizuri na hawajawakilishwa vizuri. Ni haki yao kikatiba kutoa sauti na kilio kikubwa ili Serikali iwasikize. Kwa hivyo, vijana hawa walikuwa na kilio cha haki. Walilia wakidai kwamba ukosefu wa kazi umekithiri katika The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}