GET /api/v0.1/hansard/entries/1443376/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443376,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443376/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Wanadai kwamba, Bw. Spika wa Muda, matibabu katika sehemu mbali mbali katika Jamhuri ya Kenya yamekuwa duni. Hicho ni kilio cha haki kwa sababu tumeona kwamba huduma zimedorora katika sekta ya matibabu kwa muda mrefu. Kwa hivyo, wanapolia na kusema kwamba matibabu hayako vile inavyostahili katika nchi yetu, wanaongea jambo la haki. Elimu ni jambo lingine ambalo limeleta shida katika Jamhuri yetu ya Kenya. Gharama ya kusomesha watoto imekuwa juu. Wazazi wamelia kwamba karo za shule zime enda juu. Ikizingatiwa pia vile vile, gharama ya shule za upili imepanda. Tukiingia katika vyuo vikuu, unakuta pia gharama imepanda. Kwa hivyo, wanapotoa kilio na kupaza sauti na kusema kwamba hili jambo liweze kuangaliwa, na kuzingatiwa kwa kina ni kwa sababu wako na haki na kwa jambo lolote wanalosema wanatoa kilio cha haki. Bw. Spika wa Muda, natoa wazo langu na kusema ya kwamba, Inspekta wa Polisi, Bw. Koome, amefanya jambo ambalo sisi kama viongozi, hatukukusudia. Vijana wetu wamekufa na wengine wamelazwa katika hospitali zetu. Mambo hayo yote yamesababishwa na polisi ambao walitumia nguvu kuwazuia vijana waliokuwa wanafanya maandamano ya haki. Bw. Koome, sasa ni wakati wako uweze kutoka katika boardroom ambayo umekalia sasa hivi na hata simu haushiki. Njoo uombe msamaha kwa wazazi wa vijana ambao wamepoteza maisha yao. Hili ni jambo la huzuni kubwa kwa sababu limefanyika wakati Bw. Koome ndiye Inspekta Mkuu wa Polisi katika Jamhuri ya Kenya. Tunaomba Bw. Koome ajitokeze ili aweze kuomba msamaha kwa Wakenya kwa sababu ya mauaji ambayo yametendeka katika sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Kenya. Bw. Spika wa Muda, kuna mambo ambayo pia yamesababisha shida kubwa katika nchi hii yetu. Ufisadi ni jambo ambalo limeleta matatizo na shida. Pia, ufisadi umechangia ukosefu wa kazi. Wizara tofauti zimeingiliwa na ufisadi na haziwezi kuajiri vijana wetu. Hili ni jambo ambalo linasababisha matatizo makubwa. Katika kaunti yangu ya Lamu, niko na vijana zaidi ya 100 ambao wamesimamishwa kazi katika Bandari ya Lamu. Hatujaelewa sababu na kiini cha hatua hiyo. Wameonekana kwamba ni watu wanaotoka Lamu, pengine hawastahili kuajiriwa. Jambo hilo nalilaani kwa sababu wengi waliosimamishwa kazi katika sehemu ile ni Gen Zs. Ni watu ambao tunasema kwamba tunakuja hapa kama viongozi kuwatetea wapate ajira. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}