GET /api/v0.1/hansard/entries/1443379/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443379,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443379/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Ni jambo la huzuni kubwa sana ikizingatiwa kwamba vijana hao katika Jamhuri yetu ya Kenya ndio viongozi wetu wa kesho. Ni watu wenye nguvu ambao Serikali inafaa iwalinde sana kwa sababu ndio watakaotengeneza uchumi wa nchi na Jamhuri yetu ya Kenya ili isonge mbele. Tumeona juzi kamati yetu ya Agriculture, Livestock and Fisheries ilikuja kuthathmini kashfa ya fertilizer ambayo imekumba nchi hii yetu ya Kenya. Corruptio n ambayo iko katika Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries saa hii ni kwamba lazima Serikali iaangalie jambo hili kwa kina na ione kwamba hilo jambo limeathiri Wakenya limeshughulikiwa na kuwekwa katika kaburi la sahau. Bw. Spika wa Muda, tuliona Kamati yetu ya Agriculture, Livestock and Fisheries wakija hapa kuunusa ile fertilizer kuchunguza ikiwa ni mzuri au mbaya. Hatukuweza kupata majibu ya kisawasawa kuhusu ile tathmini. Hilo ni jambo la huzuni sana kwa sababu linaweza kudororesha uchumi wetu na unarudi nyuma tukiiangalia sisi kama viongozi. Hilo ni jambo ambalo haturuhusu. Ninatoa shinikizo kwa Serikali ya Kenya. Mheshimiwa William Ruto, Wakenya wamelia sana kuhusu fertilizer . Tafadhali, fanya jambo kwa Waziri anayehusika kwa kuwaeletea Wakenya hasara kubwa sana katika Jamhuri yetu ya Kenya. Tunata Rais achukue hatua kwa sababu malalamishi ni mengi. Wananchi wanasema kwamba"
}