GET /api/v0.1/hansard/entries/1443386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443386,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443386/?format=api",
"text_counter": 156,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Nikisema ufisadi naanza na county Government hadi national Government. Ufisadi upigwe marufuku, kila mtu atosheke na mshahara wake na afanye kazi ambayo anafaa kuifanya na inavyostahili ili Kenya isonge mbele. Jambo lingine ambalo ni muhimu sana ni kwamba ni lazima tuweze kuhusisha vijana katika mambo ya kuendeleza nchi hii. Namaanisha kwamba lazima tuangalie kwamba wakati tunapofanya public participation, vijana wetu wapewe nafasi na kipaombele, waweze kutoa maoni yao na matatizo ambayo wanapitia kila uchao. Jana, nimeona kijana mmoja akiongea katika runinga. Alikuwa anatoa mawazo yake kama kijana akisema kwamba viongozi wasishinde wakiuliza ni nani anaongoza hawa Gen Zs. Hawana kiongozi ila wanaongozwa na shida na matatizo ambayo yanawakumba kila kuchao. Wanasema kwamba wale vijana wengi waliotokea hapa walikuwa wameongozwa na matatizo yanayowakumba wote kama vijana. Kwa hivyo, hao ni watu wanaofaa kusikizwa sana. Ili Serikali isonge mbele, lazima vijana wasikizwe katika public participation na mipango ya kundeleza nchi. Wasikilizwe ili tuweze ku-capture problems na needs za hao vijana. Tukifanya hivyo, tutaponya nchi hii kwa sababu hao vijana wamesoma na wako na teknolojia inayowafanya waelewe nchi inaelekea wapi. Sio Kenya pekee ila ulimwengu mzima. Hao vijana wanasema kwamba wako na references ambazo wanaweza kutoa ya nchi zingine ambayo wamefanya wanavyofanya na zikawa na mabadiliko. Kwa hivyo, jambo hili la vijana hao wetu ni la kushughulikiwa na hali ya ustaarabu kabisa na wapewe kipaombele ili maisha yasonge mbele. Namalizia kwa kusema kwamba ili Kenya isonge mbele au tuwe na hali ya usawa katika Kenya, lazima tu-provide environment ya wafanyibiashara katika Jamhuri yetu ya Kenya. Itasaidia wale wafanyibiashara ambao saa hii ni wengi katika nchi hii wapate nafasi ya kuajiri vijana. Kuprovide environment ya kufanya biashara ni kutowawekea tax ya juu ili wafanye biashara na kuajiri vijana wengi ili maisha yasonge mbele. Nashukuru kiongozi wa Walio Wengi katika Seneti. Amesifika sana kwa kuleta Hoja hii ambayo imeweza kuponya nchi au kujumuisha viongozi wote wa upinzani na upande wa Serikali kuongea kwa sauti moja. Asante. Naunga mkono."
}