GET /api/v0.1/hansard/entries/1443389/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443389,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443389/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Uchumi Samawati, jambo tulilolianza kama Kamati bila kulazimishwa ni kuhakikisha ukweli unajulikana. Seneti ina utaratibu na anayejali kusoma anajua kuna utaribu fulani. Siku ya leo ilikuwa iwe siku ya mwisho tuliyokuwa tumewaalika Waziri na washika dau wote waliohusika na haya mambo ya mbolea ili tumalize na tulete taarifa ya mwisho ya mambo yaliyotendeka. Niseme ya kwamba, tunapofanya uchunguzi, sio jambo linalochukua siku moja au mbili. Tumemaliza uchunguzi hata kabla taasisi ya usalama ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kumaliza. Kwa hivyo, hata kama sisi hatujapelekwa mafunzo, sisi tumemaliza na tarehe 21 ndio itakuwa siku ya mwisho ambayo tumewaalika kwa mkutano wa lazima. Hii ni kwa sababu hawakuja siku ya leo. Waje au wasije, tutatoa taarifa. Kama Seneta wa Kirinyaga na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, hakuna kitu tunachotarajia isipokuwa haki. Na ni vizuri tujue kwamba waliohusika katika hili janga hawafai kufichwa au kubembelezwa. Ufisadi sio jambo la maombi. Kuna shetani wa maombi na shetani wa kiboko. Ufisadi wa mbolea ni shetani wa kiboko. Tutapambana naye kwa kiboko. Pili, mambo yanayoshangaza na yalizungumziwa kidogo na Seneta wa Trans Nzoia ni kwamba katika nchi hii, tunafaa tuangalie yale mambo muhimu yaliyoangaziwa na Gen Z . Ni jambo la kushangaza kwamba unapoenda kwa vyuo vya umma, viwanja vya ndege, sehemu za burudani, vyoo vya wanaume utapata kumejazwa mipira ya kondomu za mapenzi. Lakini unapoenda kwa vyoo vya watoto wetu walio na haja yao inayokuja kwa sababu ya maumbile,huwezi kupata sodo au sanitary pads zimewekwa pale waweze kuchukua. Hii nitaiita ubaguzi wa kijinsia. Hii ni kusema ya kwamba wanaofanya uasherati wanachukuliwa kwa hali ya thamana na kupewa nafasi kubwa kuliko wale wasichana wetu wadogo, wamama na Gen Z kutumia sodo. Hivyo basi, ningeulizwa kama Seneta wa Kirinyaga ningesema tuondoe migao inayoenda kwa KeMSA kununua mipira ya kondomu ya kufanya ngono na kuwekwa kila mahali, tuipeleke kuhakikisha watoto wetu wasichana wamepata taulo za usafi ambazo kwa Kimombo ni sanitary towels . Jambo lingine, Rais amepata nafasi nzuri sana ya kuwapiga kalamu Mawaziri walio watepetevu. Wako wengi na hata wengine hawajielewi japo wako wanaojielewa. Muda kama huu ni nafasi nzuri sana ya kuwapiga kalamu ili tuwape hizo nafasi wale wanaojali na kuelewa kazi zao ili hawa Gen Z wapate wanachopigania."
}