GET /api/v0.1/hansard/entries/1443391/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443391,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443391/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "waliambiwa ni vijana na kesho. Kesho ikapita na kukaja kesho kutwa. Kesho kutwa ikapita na kukawa na mtondo na mtondogoo, kitondo na hata ikafika kitojo. Wameona siku yao haifiki na malalamishi yao hayasikizwi. Juzi, nilikuwa kwa mkutano uliokuwa na kijana mmoja aliye mhandisi wa programu za tarakilishi. Tulikutana naye mahali alipokuwa anafanya kazi ya uchukuzi na upakiaji wa mizigo katika shirika la uchukuzi la G4S. Yeye ni mhandisi. Amejaribu kutafuta kazi bila kufanikiwa. Tunapoangazia ufisadi, inafaa tuangazie hadi kwa gatuzi zetu. Ukienda kwa gatuzi yangu ya Kirinyaga, utapata kuna mgao wa asilimia 30 unaofaa kwenda kwa akina mama, vijana na walemavu. Ukienda pale kuchunguza, huwezi kupata kijana hata mmoja anayekiri ya kwamba amepata hata kandarasi moja ya kazi ya kumsaidia kimaisha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}