GET /api/v0.1/hansard/entries/1443392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443392,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443392/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Hivyo basi, naomba, pia katika gatuzi zetu ambapo pesa zinaenda kwa wingi sana, lazima tuhakikishe sheria ya ununuzi wa bidhaa inazingatiwa. Haiwezekani ya kwamba ukizunguka katika gatuzi nyingi hakuna kijana hata mmoja amefaidika. Ni wale mabwenyenye wachache wanaoandikisha wasichana wao na Gen Z wanakosa kazi. Kwa upande wa ukulima, maji ni tatizo. Kwa hivyo, hata tunapojaribu kuwapa njia mbadala na kuwaambia watafute kazi, tunasahau ya kwamba vifaa na mtaji wa kufanya kazi haupo. Ukienda kwa benki zetu, riba ni kuanzia asilimia 18 hadi 20. Wakati tunatangaza nyadhifa za kazi na kuwaambia wale vijana wawe na uzoefu wa miaka mitano, je, waliohitimu juzi kama wale walikuwa kwa barabara juzi, watatoa wapi huo uzoefu wa miaka mitano ili wapate zile nafasi za kazi? Hivyo basi, wanasikia wamekandamizwa na ndio sababu wamejitokeza kwa wingi kulalamika. Wameona hakuna kesho wasipojiunga wenyewe kuhakikisha kesho yao inapatikana leo. Ukienda kwa wale ambao wamefanya kazi na gatuzi zetu, kuna zile pesa zinaitwa"
}