GET /api/v0.1/hansard/entries/1443394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443394,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443394/?format=api",
    "text_counter": 164,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": ". Ukienda kwa Kaunti ya Kirinyaga, utapata wale walioomba mikopo kutoka kwa benki wakiwepo wanarika na kufanya kazi walizopewa, pesa zao zilizama na hata wa leo hawajawahi kuzipata. Ili wapate zile pesa, lazima watoe mlungula. Kazi ngumu ya msaraghambo na ya kutafuta fedha na kufanya kazi inakuwa haina faida. Imefikia mahali pa wale vijana kutoka nje kutukumbusha ya kwamba kuna shida katika nchi hii na lazima tuiangalie. Tukienda kwa idara ya michezo iliyogatuliwa na kuangalia pale kwetu Kirinyaga, pia najawa na huzuni. Vijana wamefanywa watu wa kucheza kandanda vijijini na malipo ni viatu na sare tu za kucheza mpira. Hakuna kitu kingine wanachopata. Tunafaa kama Seneti tuangalie ya kwamba ili vijana wawe na kazi, lazima gatuzi zetu zote ziwe na timu zinazocheza mipira hadi nyanja za kitaifa na michezo iwe ajira. Leo hii ni vijana wataenda kumenyana. Wengine wataumia. Watakaa uwanjani. Mwishowe wanapata tu viatu na sare za kuchezea mpira na maisha yanaishia hapo hadi msimu wa siasa wanasiasa wanapotaka kura. Kwa hivyo Bw. Spika wa Muda, ni jambo la maana kama wahusika wote kuanzia Serikali ya Kitaifa na zile za kaunti pamoja na sisi Maseneta tujiulize kwa undani, wewe kama Seneta, tangu uingie hapa baada ya kupewa kazi na wananchi, ni Gen Z wangapi umesaidia kupata kazi? Ni wangapi wanafanya kazi katika ofisi yako? Kuongea ni rahisi lakini lazima tufanye kazi kwa vitendo. Ukienda kwa wengi waliochaguliwa kama magavana, utapata katika ofisi mtu ameandika binamu yake au mjomba, na hawajahitimu. Wengi walioajiriwa, hawajahitimu kuliko wale vijana walioandamana juzi kwa barabara zetu. Tuliochaguliwa tulitafuta kazi tukakosa na tukaenda kwa wale wamama na vijana kuomba kazi na tukapewa. Sisi pia tunafaa kuhesabiwa kwa wale vijana tunawasaidia kupata kazi. Nikimalizia, misimamo inayohusiana na vijana wetu wa Gen Z waliokuwa juzi barabarani, lazima isikizwe. Tunajua pia kuna misimamo ya vyama na ya raia. Ninaomba tuwe tunachukua misimamo ya raia kuhakikisha wale vijana waliotupigia kura wamesaidika katika nafasi za kazi. Tuwasaidie kwa sababu, maneno waliyoyasema ni kweli. Mwisho, huwa naona wakati ukifika wa kuwasajili makurutu wa jeshi au National"
}