GET /api/v0.1/hansard/entries/1443397/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443397,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443397/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "watokelezee 1,000 halafu tunawachukua watano tu. Lazima tutafute njia mbadala ambayo hata kama ni ya kiteknologia ili wale ambao wanatafuta zile ajira watakuwa wanafanya zile application pale kabla ya kufika uwanjani, ili tuweze pia kumaliza kabisa ufisadi unaoendelea na pia ubaguzi wakati wa kupeana kazi. Kwa hivyo, mimi kama Mwenyeketi wa Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati, yaliyosemwa nimeyasikia na nimeahidi ya kwamba sisi tumefanya msaragambo au kazi ngumu na tumemaliza. Tarehe 21 tumewaita wale washikadau wote kuhakisha kwamba tumemaliza ile taarifa ya upelelezi ya mbolea gushi. Tutakuja kuiwasilisha hapa na tumefuata Katiba na sheria zote za Seneti ambazo zimewekwa ili tuweze kuhakikisha kwamba tumefanya kazi inayofaa na tutaleta taarifa ambayo ni ya kweli bila kuficha chochote. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}