HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443434,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443434/?format=api",
"text_counter": 23,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "shirika la Elimu na Sayansi na Utamaduni wa umoja wa mataifa UNESCO ili kuadhimisha lugha ya Kiswahili kila mwaka kuanzia mwaka wa 2022. Chimbuko la Kiswahili ni Afrika Mashariki. Kwa sasa, lugha hii inazungumzwa kwa mataifa kumi na nne ikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Sudan Kusini, Msumbiji, Malawi, Zambia, Comorros, Oman na Yemen katika Mashariki ya Kati. Vilevile, lugha ya Kiswahili imeanza kufunzwa katika shule za Afika Kusini na baadhi ya vyuo vikuu nchini Japan na China. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ilikuwa ni, “Elimu na Wingi Lugha katika ufanikishaji wa Amani Ulimwenguni.” Washikadau wakisema ipo haja ya kuikuza lugha ya Kiswahili na kuitumia kueneza amani katika baadhi ya nchi zinazounda jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuna maeneo mengi katika jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo yana ukosefu wa amani ikiwemo Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Sudan Kusini na Somalia. Iwapo wananchi wataungana chini ya mwavuli wa wa lugha moja ya Kiswahili, amani ya kudumu na maendeleo yatapatikana katika nchi hizo. Tukirudi hapa nyumbani, hususan katika Seneti, tulipiga hatua kadhaa katika kupanua matumizi ya Kiswahili hapa Bungeni hadi kufikia hatua za kutafsiri Kanuni za Kudumu za Bunge hili kwa lugha ya Kiswahili. Tulitarajia ya kwamba hatua zengine zitafuata pamoja na kutafsiri Miswada ya sheria kwa lugha ya Kiswahili ili wakenya waweze kusoma sheria hizo na kuzielewe mara zinapojadiliwa Bungeni. Hata hivyo jambo hilo halijafanyika. Labda ni ndoto iliyo mbali kutimia. Inalazimu Bunge ifanye mikakati ya kukikuza Kiswahili kwa sababu ni lugha ya kiafrika na ndiyo lugha pekee inayotu unganisha kama wakenya. Hatujafaulu kuitumia kikamilifu upana wa lugha ya Kiswahili. Seneti kama baba na mlinzi wa ugatuzi, tuna jukumu kubwa la kutekeleza kwani lugha ni muhimu katika vyombo vya mawasiliano na katika huduma zilizogatuliwa. Kufaulu kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili kutafanikisha ugatuzi kwa vile itakuwa ni rahisi kufuatilia mambo ya maendeleo. Mbali na hayo, niliwasilisha Hoja moja iliyochapishwa kwa Kiswahili katika Seneti mnamo tarehe ishirini na tatu, mwezi wa n ne, mwaka huu. Hoja hiyo iliungwa mkono na Maseneta kumi ambao wote waliongea kwa lugha ya Kiswahili. Hatimaye, Hoja hiyo ilipitishwa kwa wingi wa kura ishirini na saba. Jambo la kutia moyo ni kwamba, kila Seneta aliyesimama alikuwa tayari kuchangia Hoja hiyo kwa lugha ya Kiswahili. Mhe. Spika, maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani yalifanyika Mombasa, Kenya mwaka huu. Kilele cha maadhimisho hayo ilikuwa jumapili, tarehe saba, mwezi huu wa saba ambapo waziri wa Jinsia na Utamaduni, Mhe. Aisha Jumwa, alitoa hotuba rasmi. Jambo la kutia moyo ni kwamba wageni wote waliohutubu walitumia lugha ya Kiswahili. Kulikuwa na Jaji kutoka Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki na wengineo. Wote walizungumza kwa lugha ya Kiswahili. Baadhi ya maazimio ya Kongamano hilo ni kuzinduliwa rasmi kwa Taasisi ya Lugha ya Kiswahili ambayo itakuwa na jukumu la kufanya utafiti zaidi wa masuala ya lugha ya Kiswahili na kuboresha lugha hii. Kuna mambo mengi ibuka ambayo yanapaswa kufanyiwa utafiti. Kwa mfano, neno “Gen Z,” tunafaa kuwaita vipi kwa lugha ya Kiswahili. Kuna maneno mengine yaliyoibuka kama Artificial Intelligence . The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}