GET /api/v0.1/hansard/entries/1443435/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443435,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443435/?format=api",
    "text_counter": 24,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kwa Kiswahili inajulikana kama akili nemba ama akili unde. Masuala hayo hatuwezi kuyajua kama hatujapata taasisi kama hii itakayofanya utafiti. Lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya lugha zinazokuwa kwa kasi mno. Hivyo basi, kuwepo kwa taasisi hiyo kutasaidia pakubwa kudhibiti lugha hii. Nikimalizia, ningependa kutambua mchango wa ndugu yetu mtangazaji Nuhu Zuberi Bakari ambaye juzi alitoa shairi kuhusu Gen Z . Shairi hilo lilisambaa kwa kasi mitandaoni na kuwatia vijana moyo. Vile vile, ningependa kutambua mchango wa vijana wetu malenga katika Kaunti ya Mombasa, wakiwemo Mwagarashi, Mwakaga, Malenga 001, na wengine wengi ambao hutunga mashairi katika hafla mbali mbali. Hiyo inachangia pakubwa kukuza lugha ya Kiswahili. Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii. Viva Kiswahili."
}