GET /api/v0.1/hansard/entries/1443447/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443447,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443447/?format=api",
    "text_counter": 36,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
    "speaker_title": "The Senate Majority Leader",
    "speaker": {
        "id": 13165,
        "legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
        "slug": "aaron-cheruiyot"
    },
    "content": " Bw. Spika, ningependa kuungana na Seneta wa Kaunti ya Mombasa ambaye leo ameamua kutuhamasisha kuhusu lugha ya Kiswahili na matumizi yake nchini Kenya. Mara nyingi, sisi kama taifa na hasa viongozi huzungumza lugha hii kwa urahisi. Hata hivyo, unapopewa fursa kama hii kutumia lugha hii kwa usahihi ili watu wakusikilize, watu wengi wanapiga kona. Siku ya Kiswahili iliadhimishwa ili kuhakikisha kuwa matumizi yake yanajulikana katika taifa letu. Hiyo ni siku ya maana sana. Jambo linaloleta changamoto ni kuwa hadi sasa, kando na viongozi wachache kutoka kaunti ambazo zinatumia lugha hii katika shughuli zao za kila siku, hatuoni Serikali ikiwa mstari wa mbele kuipa siku hiyo kipaumbele ili kuhakikisha kwamba taifa lote linajua maana yake ili kupata umaarufu duniani. Ikiwa unafuatilia mambo yanayoendelea duniani, utafahamu kuwa mataifa mengi yameruhusu wananchi wao kujifunza Kiswahili. Kwa mfano, Japani, Uchina, na Marekani. Utapata wanafunzi wa lugha ya Kiswahili huko. Wanafanya vile wakijua kuwa siku moja wakiwa katika kazi zao au starehe na likizo wataweza kuzuru maeneo ya Afrika Mashariki ambapo lugha hii inatumika kwa wingi. Kwa hivyo, itawabidi kutumia lugha ya wenyeji. Katiba yetu inatambua kwamba nchi yetu ina lugha mbili rasmi; Kiingereza na Kiswahili. Hata hivyo, mara nyingi maelezo yanayopeanwa kuhusu shughuli mbalimbali za Serikali hutolewa kwa lugha ya Kiingereza. Juzi kulipokuwa na hali ya suitofahamu nchini iliyosabisha kelele na rabsha zilizotokea kutokana na kupitishwa kwa Mshada wa Fedha katika Bunge la Taifa, nilisikia wananchi wakizungumza katika redio. Hiyo ilikuwa baada ya Rais kueleza yaliyokuwa yamependekezwa katika Mswada huo. Wengi walisema kuwa hatukuwa tumewaeleza. Kuna jamaa mmoja aliyepiga simu katika redio na ninakubaliana naye. Alisema kuwa Mswada huo ulikuwa umechapishwa katika lugha ya Kiingereza pekee. Kwa hivyo, wazee wangeelewa vipi? Aliendelea kusema kuwa walikuwa wanafuata mambo ambayo wananchi wengine walikuwa wakisema. Tunaishi katika mfumo wa kidigitali. Mara nyingi watu hufuata yale wananchi wengine wananena bila kujua kama ni ukweli au uongo. Kama Wabunge, lazima tujizatiti ili kuhakikisha kwamba tunapoleta Miswada hapa, ikiwa watu wengi wataathirika kwa njia moja au nyingine, tunafaa kuhakikisha kuwa Miswada hiyo imechapishwa kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili. Endapo tungefanya hivyo, pengine wananchi wengi wangelewa mambo yaliyokuwa yanazungumziwa kwenye Mswada huo. Nakubaliana na Sen. Faki katika Taarifa aliyoleta. Sisi kama viongozi wa Bunge la Seneti tunafaa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Kiswahili hakisahauliki. Kuna The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}