GET /api/v0.1/hansard/entries/1443448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443448,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443448/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
"speaker_title": "The Senate Majority Leader",
"speaker": {
"id": 13165,
"legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
"slug": "aaron-cheruiyot"
},
"content": "wananchi wengi sana ambao hawaelewi lugha ya Kimombo. Wanaelewa lugha ya mama au Kiswahili pekee. Kama viongozi wao, ni vizuri tujifunze lugha hii hata hapa katika Seneti. Sijui kwa nini katika kipindi hiki hatujazingatia maneno hayo. Katika siku zangu za kwanza kwenye Seneti, siku ya Alhamisi ilikuwa imetengwa kuwa ya Kiswahili. Maseneta wote walikuwa wanajizatiti kuhakikisha kuwa wanatoa michango yao kwa lugha ya Kiswahili. Wengi walikuwa wanajikaza kweli kweli. Mtu angefanya makosa hapa na pale na hatimaye wakaanza kuzoea. Baada ya muda mchache, ilikuwa jambo la kawaida. Ilipokuwa ikifika Alhamisi, Maseneta wote walikuwa wanachangia kwa lugha hii. Hatuwezi kuwa na Kiswahili na Kiingereza kama lugha rasmi za taifa ilhali kila siku tunazungmza Kiingereza pekee. Kwa hivyo, napendekeza rafiki yangu Sen. Faki apendekeze marekebisho kwenye Kanuni zetu za Kudumu ili tuwe na siku moja ya kuzungumza Kiswahili. Pengine hiyo itatusaidia kupunguza hoja za nidhamu kila wakati kwa sababu wakijua kuwa unafaa kuzungumza kwa lugha ya kiswahili, hawatataka kuzungumza ovyo ovyo. Lazima uhakikishe kuwa una maneno ya kutosha kujieleza na mambo kama hayo. Bw. Spika, hivyo tutakuwa tumehakikisha ya kwamba taifa letu limekuza Lugha hii kwa sababu mataifa mengine ambayo yanatumia Kiswahili, mbali na kujifunza Lugha ya Kifaransa ama Lugha ya Kiingereza, wanazidi kufanya mikakati kuhakikisha kwamba kulingangana na desturi, kanuni na mila zetu, Kiswahili hakijapotezwa. Kwa hayo mengi, ninashukuru na ninafikiria nimeongea Kiswahili mufti na sanifu. Kwa hivyo ninaomba nipigiwe makofi kabla ya kukaa"
}