GET /api/v0.1/hansard/entries/1443451/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443451,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443451/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Ningependa kumpa ndugu yangu Sen. Cheruiyot heshima sana kwa sababu amejaribu kuzungumza lugha hii. Hata hivyo, unapomsikia anavyotamka majina ya Kiswahili, utaelewa kuwa kuna mengine ambayo ameyasoma na kuna mengine ambayo alikaa jana usiku akakaa na kuyaangalia kabisa. Hata hivyo, ni heshima kuskia akijieleza vile alivyojieleza. Ningependa pia kumpa heshima zangu Sen. Faki, mzee ambaye tunamheshimu. Mimi nina bahati sana kwa sababu nilipokua ninakuzwa, mamangu na mzee wangu walikuwa wanazungumza Kiswahili nyumbani. Bahati hiyo ndiyo iliyonifanya nikaelewa mambo mengi sana. Jambo la pili, wakati ambapo tulianza kusoma na miaka yangu sio mbali sana na yako, enzi zile watoto wengi sana kama vile mimi kutoka maeneo ya Kisii walikuwa wanapelekwa kusoma Kwale. Watoto wa Kwale walikuwa wanasafiri, kama mimi. Nilienda kusoma katika shule ya wavulana ya St. Mary’s Yala. Tulikuwa na vijana Wajaluo, Wagiriama na Wataita kwa hivyo ilikuwa ni lazima tujifunze lugha ambayo tutajizungumzia na kujielezea. Ni viruzi kwa ndugu zetu kuanza kuzungumza na kukubali kuwa lugha ya Kiswahili ni msingi wa desturi yetu. Lugha ya Kisahili ni lugha ambayo ina mambo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}