GET /api/v0.1/hansard/entries/1443452/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443452,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443452/?format=api",
    "text_counter": 41,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "matatu makubwa. Kwanza, unajieleza vilivyo, pili inaleta uuiyano; ukishaleta uuiano, unaweza kufanya biashara. Ni lugha ambayo uki zungumza, hata ukisema “pole, sikukusudia kukukanyaga” mtu anaelewa na ajua kiroho hatasikia vile ulivyomuumiza. Ningependa kumsifu ndugu yangu Sen. Faki na ningependa kuwauliza vile ndugu zangu wamesema, Jumba hili tujaribu kuhakikisha kuwa tunaikuza lugha ya Kiswahili ili majadiliano yetu na mambo yale ambayo tunazungumza katika Jumba hili, wananchi wengi wapate nafasi ya kusikiliza na kuelewa ni nini kinachoongelewa. Jambo la pili, ningependa kumuuliza Sen. Faki kuwa aanze kufikiria vile tutakavyoweza kuhakikisha kuwa shule zetu--- Mwaka uliyopita, nilikuwa na kijana wangu ambaye alifanya mtihani wa Kidato cha Nne. Kilichonishtua ni kuwa alipita kila kitu ila Kiswahili. Nilishtuka kwa sababu mimi nilikuwa ninapita Kiswahili na kuanguka Hesabu, au Sayansi. Nilijiuliza ni kwa nini lugha ya Kiswahili haijapewa umuhimu kule shuleni ili wanafunzi wetu wasione kuya hiyo ni lugha ya ulaghai, ukora, na ya wale ambao hawajiwezi. Wajue umuhimu wa lugha hii kwa sababu lugha hii ni historia yetu, desturi yetu, ni nyimbo zetu na ni lugha ambayo tukiikuza na tuifanye iwe lugha ambayo sisi sote tumeikubali, italeta uuiano kwa inchi yetu na itatuwezesha kufanya kazi vizuri pamoja na viongozi wetu kwa sababu tukiwa kule mashinani, mtu huwa anaanza kuongea kwa Kizungu halafu anaingia katika lugha ya mama. Tukiweza kufanya hivyo na kurekebisha hayo, tuwe tunaongea kwa lugha ya Kizungu lakini, pia tuipatie umuhimu lugha ya Kiswahili kwa sababu hii pia ni lugha ya mama na ndiyo lugha ambayo waafrika wengi sana wanaongea wakati huu. Asante kwa kunipa nafasi ili nichangie mjadala huu wa muhimu."
}