GET /api/v0.1/hansard/entries/1443455/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443455,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443455/?format=api",
    "text_counter": 44,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Kiswahili inaongelwa katika inchi za Japan, China na hapa Afrika, na kama alivyosema, nchi zaidi ya kumi na nne. Kwa hivyo, tuendelee kukiimarisha Kiswahili hususan hapa Bungeni kwa sababu sisi tunaongea na watu wengi katika jamhuri ya Kenya Katika Bunge lililopita, ninakumbuka kila siku ya Alhamisi, aliyekuwa Spika wa Muda ambaye sasa ndiye anaongea kwa niaba ya Serikali, Mheshimiwa Mwaura, kila wakati alipoketi pale kwenye kile kiti, kila mtu alikuwa anaongea kwa lugha ya Kiswahili. Ingekuwa ni vizuri zaidi. Ninachukua nafasi hii kupongeza Kaunti ya Laikipia haswa Bunge la gatuzi hilo. Lilikuwa la kwanza kutafsiri Kanuni zake za Bunge kwa Lugha ya Kiswahili na wale wengine wakachukua mkondo huo. Na sasa vile ambavyo Sen. Faki amejitokeza na kusema ya kwamba Kiswahili kitukuzwe, mimi ninamuunga mkono na ninaomba tuwe na siku, vile alisemavyo kiongozi wa walio wengi, tutenge siku ya Kiswahili. Bw. Spika wewe umebobea katika lugha ya Kiswahili, hatuna shaka. Siku yoyote ambayo tutaitenga, wewe utakuwa chonjo, utakuwa ngangari na sisi tuweze kuendeleza lugha ya Kiswahili. Ni vizuri kwa sababu, hakuna Mkenya ambaye hataweza kuelewa vile tunavyosema. Wakati Sen. Sifuna na Sen. Crystal Asige wanapoongea kwa lugha ya Kiingereza pengine nusu ya wakenya hawaelewi kirasmi. Lakini Sen. Faki au Sen. Madzayo wanapoongea kwa lugha ya Kiswahili, wakenya wataelewa kwa haraka na hautaambiwa ujieleze kwa sababu watakuwa tayari wameyapata. Asante kwa kunipa fursa hii, na Kiswahili Kitukuzwe."
}