GET /api/v0.1/hansard/entries/1443461/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443461,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443461/?format=api",
"text_counter": 50,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Ninachukua nafasi hii niweze kujumuika na Seneta mwenzangu wa kutoka katika Jimbo la Mombasa, Sen. Faki kwa kuunga mkono swala hili ambalo amelileta siku ya leo, ya kwamba, Kiswahili kitukuzwe katika Jamhuri yetu ya Kenya. Bw. Spika, nimefurahishwa na Taarifa ambayo ametoa siku ya leo. Ni vizuri ibainike ya kwamba, tunapofanya campaign katika Jamhuri yetu ya Kenya, sisi hutumia lugha ya Kiswahili ili wananchi waweze kuelewa ni mambo gani ambayo tutaweza kuwafanyia tukichaguliwa. Tunapofika katika Bunge, Miswada inachapishwa kwa lugha ya Kingereza. Jambo hilo huwa linatatiza wananchi wetu tunao waakilisha ikizingatiwa kwamba, kuna asilimia kubwa ambao hawakupata fursa ya kupata elimu. Ni vizuri pia kwa sababu ni Wakenya na wapiga kura, waweze kupata fursa ya kuelewa ni nini kinachoendelea katika Jamhuri yetu ya Kenya. Naunga mkono nikisema ya kwamba, ni vizuri tunapoendeleza nchi, tuzingatie watu wote; wale ambao wako na uwezo wa kielimu na wale pengine kidogo, hawakufanikiwa kufaulu kielimu. Kwa hivyo tukiweka hali zetu za utaratibu wa Bunge katika lugha ya Kiswahili, itawafaa na wataweza kufuata vile gatuzi zetu zinavyo endelea katika Jamhuri nzima ya Kenya kwa jumla. Bw. Spika, kwa hivyo naunga mkono jambo hilo na Kiswahili kitukuzwe. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}