GET /api/v0.1/hansard/entries/1443464/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443464,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443464/?format=api",
"text_counter": 53,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisang’",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika. Nachangia hii Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Gatuzi la Mombasa. Unajua ya kwamba, wengine wetu hatukusoma 8-4-4. Wakati wetu, haikuwa lazima tufanye Kiswahili katika kidato cha nne. Mimi nilisoma Kiswahili katika Darasa la Sita term moja na Form One term moja. Kwa sasa, najikaza na kusema ni vizuri kama Seneti, tuwe tukiongea Kiswahili kwa sababu sheria yetu inasema Kiswahili na Kingereza ni lugha za Kitaifa. Nafikiri ni vizuri hata tukiongeza lugha ya mama kwa sababu tukiwa katika darasa la kwanza, la pili na la tatu, tulikuwa na kitabu tulichokuwa tukisoma kilichoitwa T.K.K. Na ilikuwa ni lazima. Wakati huu, watoto wetu hawaelewi lugha ya mama. Nafikiri ni vizuri tuongeze lugha ya mama. Wakati luhga ya Kiswahili ilikuwa ikisherehekewa Jumapili iliyo pita katika dunia yote, haikupewa kipao umbele kwa sababu tumekichukua Kiswahili kama lugha ambayo sio ya maana. Unajua ya kwamba, Community yetu ya Afrika Mashariki wanaelewa na kuongea Kiswahili. Kwa hivyo, ni vizuri tujizoeshe. Mwisho, nataka kuchangia Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Gatuzi la Marsabit. Ukienda kwa gatuzi zetu, madaktari interns ndio wanafanya kazi. Kwa hivyo, tunashangaa ni kwa nini gatuzi zetu haziwalipi pesa kwa wakati unaofaa na wakati pesa inapatikana waajiri wale ambao wamekuwa interns kwa mda mrefu. Nafikiri Kiswahili changu kinaishia hapo. Nimejikaza sana."
}