GET /api/v0.1/hansard/entries/1443466/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443466,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443466/?format=api",
"text_counter": 55,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Kwanza, nasimama kumuunga mkono Seneta wa Mombasa, Sen. Faki, kwa kuleta hii Taarifa katika Seneti. Kule niliposoma, tulikuwa tunatilia maanani sana somo la Kiswahili. Ukiwa mwanafunzi shupavu, ilikuwa lazima uwe umenoga katika kuzungumza lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, nawasihi ndugu na dada ambao wako katika shule, wajivunie kuzungmuza lugha ya taifa kwa sababu Kiswahili ni lugha ya taifa. Seneta wa Embu, Daktari Mundigi, akisimama kuchangia, yeye huongea lugha ya Kiswahili. Nilipomuuliza mbona, alisema ya kwamba, wakaazi wengi wa Jimbo la Embu wanaelewa Kiswahili. Kwa hivyo, akizungumza lugha ya Kiswahili, huwa wanampata moja kwa moja. Kwa hivyo, naomba wanafunzi wetu shuleni wajivunie kuzungumza lugha ya Kitaifa. Nilishangaa siku moja nilipotembea kule Oman kumuona rafiki yangu Monte ambaye tulisoma naye. Nilipofika kule na kuchukua taksi ili niende kumuona yule rafiki yangu, nilishangaa sana kwamba, wale ambao wanaendesha taksi, wanazungmza Kiswahili sanifu kuliko tunachokizungumza huku Kenya. Kwa hivyo, nawaomba watoto wetu katika vyuo mbali, wajivunie kuzungumza lugha ya Kiswahili. Hata ukiangalia wale ambao walipigana kutupea Katiba katika mwaka wa 2010, walihakikisha kwamba, ile lugha ambayo inatambulika katika Bunge ni lugha ya kizungu, Kiswahili na ishara ili ukishindwa kuzungumza kizungu au Kiswahili, unaweza kuzungumza kutumia ishara. Jitihada ambayo tunahitaji kufanya ni kufuatilia yale ambayo wale walitupa Katiba mpya walitaka. Tayari, wametambua lugha ya Kiswahili katika Katiba. Inatakiwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}