GET /api/v0.1/hansard/entries/1443467/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443467,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443467/?format=api",
    "text_counter": 56,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omogeni",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13219,
        "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
        "slug": "erick-okongo-mogeni"
    },
    "content": "sasa sisi kama viongozi tuhakikishe kwamba Miswada ambayo inakuja katika Bunge inachapishwa katika lugha ya kizungu na Kiswahili. Bw. Spika, kuna wengi ambao wangependa sana kusoma Mswada wa Fedha, 2024 ambao ulikuwa unajadiliwa katika Bunge la Kitaifa. Lakini, kwa sababu umechapishwa kwa Kiingereza, kuna wengi hawapati faida ya kuusoma huo Mswada. Kwa hivyo, tuweke bidii, tuhakikishe kwamba hii Miswada ikichapishwa katika lugha ya kizungu, pia tunaichapisha katika lugha ya Kiswahili ndiposa tuweze kukuza lugha ya Kiswahili. Waswahili wanasema tumemla ng’ombe mzima, mkia umetushinda. Hii ni kwa sababu, tukiweka hii Miswada katika Kiswahili, tutakuwa tumemla ng’ombe pamoja na mkia wake. Naomba wale wenzetu wanaozungumza lugha ya Kiswahili, wasiongee tu hapa wakisema wanataka kukuza lugha ya Kiswahili kisha wakitoka nje, wanaongea lugha nyingine. Wanasema kwamba tutende yale ambayo tunasema. Hata tukiwa katika Bunge alafu Seneta wa Laikipia, Sen. Kinyua, anipate, awache tuzungumze lugha ya Kiswahili. Hii itasaidia wengi wetu kuimarisha mazungumzo yetu katika lugha ya Kiswahili. Tusipofanya hivyo, itakuwa kama vile waswahili wanavyosema; kibogoyo anamcheka yule aliye na mapengo. Kwa hivyo, inatakiwa uhakikishe kwamba, ukimkuta Seneta wa Kisumu, Sen. Ojienda, unamzungumzia katika lugha ya Kiswahili. Bw. Spika, naunga mkono na naomba kama inawezekana, tuteuwe jopo maalum la kuangalia ni vipi Hoja zetu zikija kwenya Bunge, zinachapishwa katika lugha ya Kingereza na pia Kiswahili. Vijana wale wako shuleni, watajua kwamba, hata wakitaka kumtafuta mke, sio lazima wamuongeleshe katika lugha ya Kingereza. Mimi mwenyewe, ili nimpate mke wangu, nilimtungia shahiri la Kiswahili. Nikamwambia; “mpenzi wangu nimpendaye Jackline”. Hiyo ndio ilifanya nikapata mke wangu. Kwa hivyo, isikuwe kwamba vijana wakizungumza na wapenzi wao, wanawazungumzia kwa lugha ya Kiengereza. Pia, lugha ya Kiswahili inaweza kumtoa nyoka pangoni. Kwa hivyo, naunga mkono hii Taarifa iliyo letwa na Mheshimiwa Faki na nahimiza Maseneta wenzangu wajaribu kutilia mkazo kukuza lugha ya Kiswahili. Wanasema kwamba; muacha mila ni mtumwa, kwa hivyo, tulinde mila zetu na lugha ya Kiswahili ili iweze kuwa na mizizi katika nchi yetu."
}