GET /api/v0.1/hansard/entries/1443469/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443469,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443469/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Tabitha Mutinda",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono Seneta wa Mombasa, Sen. Faki, kwa Taarifa aliyoleta kuhusu Siku ya Kiswahili Duniani. Ningependa kuanza kwa kusema kwamba nilipokuwa mwanafunzi, Kiswahili ni mojawapo ya masomo ambayo nilipata alama za juu sana. Kwa hivyo, najivunia Kiswahili. Ningependa kuwatambua Maseneta ambao wamekuwa wakizungumza Kiswahili hapa. Miongoni mwao, kuna Sen. Faki wa Mombasa, Sen. Kinyua wa Laikipia na Sen. Mwaruma. Vile vile kuna mwenzangu Sen. Mundigi wa Embu ambaye ameimarisha matumizi ya Kiswahili. Mwingine ni Sen. Madzayo ambaye amekuwa mstari wa mbele. Tunawashukuru na wazidi kuendelea. Ni ishara njema ya uongozi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}