GET /api/v0.1/hansard/entries/1443470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443470,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443470/?format=api",
"text_counter": 59,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Tabitha Mutinda",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Jambo lingine ni kwamba ni vizuri ofisi zote za Serikali na zisizo za Serikali zihimize matumizi ya alama katika Kimombo na vile vile Kiswahili. Katika Kimombo, inajulikana kama signage . Hiyo ni ishara kwamba lugha zote mbili zinatambulika katika nchi hii. Pia sheria zetu ziwe katika lugha zote mbili. Hiyo itafanya watu waimarishe lugha zote. Ni kama tunasisitiza matumizi ya Kimombo. Utapata kuwa vitabu vinavyotumika au sheria zetu ziko katika lugha ya Kimombo pekee. Kwa hivyo, Kiswahili kitaachwa nyuma kama lugha. Kiswahili ni lugha ya heshima sana ukizingatia utaratibu wake. Siku hizi ni nadra sana kupata watoto wetu wakijieleza kwa Kiswahili. Somo la Kiswahili limerudi nyuma sana. Kwa sababu ni lugha inayounganisha Afrika Mashariki, ni vizuri kuhimiza watoto wetu kuipenda. Wataimarika ikiwa tutawaonyesha mfano sisi kama wazazi na viongozi tunapozungumza Kiswahili. Nakubaliana na Sen. Omogeni kwamba lugha ya Kiswahili ni nyororo na tamu sana. Unapoitumia kujieleza kimapenzi, inanyoosha maneno kabisa. Napenda nyimbo za Bongo. Lugha ya Kiswahili inafanya ujumbe unaopitishwa kuingia hadi kwenye mishipa. Kwa hivyo, naunga mkono. Tuzidi kusema kwamba Kiswahili kitukuzwe."
}