GET /api/v0.1/hansard/entries/1443472/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443472,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443472/?format=api",
    "text_counter": 61,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, nashukuru Sen. Faki kwa kuzua mjadala kuhusu jinsi Seneti inafaa kuwa inatumia Kiingereza na Kiswahili. Namshukuru kwa sababu mimi ni mmojawapo wa wale wanaozungumza Kiswahili kila wakati. Huwa najivunia sana ingawa watu wengine nchini Kenya na sehemu zingine hunicheka. Najikakamua kuongea Kiswahili kwa sababu naamini kuwa watu wa Kaunti ya Embu waliponichagua walijua kuwa Maseneta huzungumza Kiswahili au Kiingereza. Hata ninapotumia Kiswahili, nimesaidia sana watu wa Kaunti ya Embu. Simaanishi kuwa watu wa Embu hawana elimu ya kutosha kwa kuwa wamesoma vizuri sana. Ninapozungumza Kiswahili, huwa nataka kuhakikisha kuwa kila mtu kule mashinani ambaye haelewi Kiingereza ananielewa. Wakati ninapoenda vijijini, kila mtu huniambia kuwa anapendezwa na jinsi ninavyozungumza Kiswahili. Ningependa Maseneta wenzangu wafahamu hili. Mwaka wa 2007, niliwania kiti cha Mbunge wa Gachoka. Kwa sasa eneo Bunge hilo linajulikana kama Mberee South . Wakati huo, Wabunge walikuwa wanazungumza Kiswahili na Kiingereza. La ajabu ni kuwa watu waliokuwa wamesoma sana walikuwa wanaenda kufanya mitihani ya Kingereza na Kiswahili pale Jogoo House. Wengi walikuwa wakitemwa nje kwa sababu hawakujua kuongea Kiswahili. Bw. Spika, mimi ni miongoni mwa wale wanaounga mkono Sen. Faki, Seneta wa Kilifi na yule wa Lamu. Mara nyingi wamekuwa wakizungumza Kiswahili katika Seneti. Ningependa watu wa Embu wafahamu kuwa haimaanishi kwamba sijui Kiingereza. Ninapozungumza Kiswahili, huwa naongea kwa utaratibu kwa lugha ambayo mwananchi kule mashinani anaelewa. Embu ina maeneo Bunge manne. Kutoka Makutano hadi Kathageri na Irangi hadi Kiambere, watu wengi wamesoma. Nazungumza Kiswahili kwa sababu mimi ni mtetezi wa watu wa Kaunti ya Embu. Kuna mambo ya wakulima na hata watu wanaofanya kazi zingine. Kwa hivyo, mara nyingi nazungumza Kiswahili na nitazidi hivyo hivyo kwa sababu najua wananisikia hata saa hii. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}