GET /api/v0.1/hansard/entries/1443475/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443475,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443475/?format=api",
    "text_counter": 64,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii ili niongeze sauti yangu kwa kuunga mkono Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Mombasa. Ni muhimu kusherehekea Siku ya Kiswahili Duniani kwa maana ni lugha ya taifa ambayo inaeleweka kwa kila familia, shuleni na mahali popote. Kiswahili ni lugha muhimu kwa sababu watu walioenda shuleni na wale ambao hawakuenda shuleni wanaweza kukizungumza na kuelewana. Tunapotumia Kiswahili hapa katika mijala yetu ama mambo yanayowahusu Wakenya, kila mtu, akiwemo nyanya yangu kule nyumbani, anaelewa ninachozungumzia kwa kuwa Kiswahili ni lugha inayokaribiana na lugha za kibantu au lugha nyingi za Kiafrika. Kiswahili ni lugha safi inayoeleweka na kuvutia kwa mnenaji na anayesikiliza. Kwa hivyo, ningeomba kwa kweli tuwe na siku ya kuzungumza Kiswahili. Tunapozungumza Kiswahili kama vile Seneta wa Embu ameeleza, hakika watu waliomchagua ama wanaotupatia nafasi za uongozi, kila mmoja ataweza kufuatilia mazungumzo tunayotoa na kuelewa bila kuuliza wengine wamuelezee. Kiswahili ni lugha raisi. Hata shuleni, ni vigumu sana kupata mwanafunzi ambaye analemewa kabisa hata kama hajasoma kwa mtihani wa Kiswahili. Kwa hivyo, ni lugha ambayo tunapaswa kuiunga mkono na kuitumia sana hasa sisi viongozi ili wale tunaowawakilisha waelewe kila jambo ambalo tunazungumzia. Lugha ya Kiswahili mtu anaweza izoea na kuongea hata kama hawezi andika Kiswahili sanifu lakini kwa kuongea itakuwa ni rahisi kuliko lugha zingine zinazotumika. Kiswahili kiko na maneno ambayo hayawezi kueleweka kwa lugha nyingine. Kama unataka kupamba na kuweka maneno matamu kwa mwanamke mrembo kama Seneta wa Kaunti ya Nakuru, utatumia Kiswahili ambacho kitaonyesha ukweli wa urembo, mwenendo tabia zake na mambo anayofanya ikiwa rahisi sana kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, Bw. Spika naunga mkono Hoja hii ya kuwa na siku ya kuzungumza Kiswahili. Asante sana."
}