GET /api/v0.1/hansard/entries/1443478/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443478,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443478/?format=api",
    "text_counter": 67,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kathuri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13590,
        "legal_name": "Murungi Kathuri",
        "slug": "murungi-kathuri"
    },
    "content": "zaidi ya dakika 15. Nakushuru ili tuweze kuongoea na kufuatilia utaratibu huu wa Kiswahili. Nikiwa katika Bunge la Taifa, siku ya Alhamisi mchana kutoka saa nane, kwa muda wa miezi mitatu, kila Mbunge alikuwa anaongea kwa lugha ya Kiswahili. Pia nimesikia Seneta wa Kericho ambaye pia ni Kiongozi wa Walio Wengi akisema siku ya Ijumaa wakiwa Seneti walikuwa wanaongea lugha ya Kiswahili. Labda ameshindwa kujua Alhamisi kwa Kiswahili akasema Ijumaa. Nadhani alikuwa anasema Alhamisi mchana pia wao walikuwa wanachangia masuala yote ya Seneti kwa lugha ya Kiswahili. Hivyo basi, pia sisi tunaweza kubadilisha Kanuni zetu za Kudumu pia tuweke siku moja kwa wiki kama Jumatano asubuhi au saa nane ama Alhamisi saa nane ili tuwe tunaongea Kiswahili ili tukuze lugha yetu ya Taifa. Pia, wale watu waliotuajiri hapa wengi wanaelewa lugha ya Kiswahili. Mambo mengi tunayoyazungumza hapa ni yale yanayolenga wale waliotuchagua - walioko mashinani. Wanaposikia tukiongea Kiswahili, wanaweza kufuatilia vizuri. Kuna viongozi Maseneta wamekuwa hapa wakiongea Kiswahili kama vile Kiongozi wa Walio Wachache, Sen. Mwaruma, Sen. Munyi Mundigi na Sen. Faki mwenyewe. Sen. Tabitha Mutinda amezungumzia vile yeye hutumia Kiswahili lakini ni kidogo kidogo. Sio mara nyingi yeye huongea Kiswahili hapa. Namtia moyo sasa kutoka leo aongee zaidi kwani sio siku zote yeye hutumia Kiswahili. Hivyo basi, kutoka leo, nimeamua sasa natumia lugha ya Kiswahili. Yule naona yuko kwa shida kubwa ni Seneta wa Migori kwa sababu sijui kama anakifahamu Kiswahili na wengine hapa pia. Bw. Spika, nakushuru kwa muda huu uliotupa kuzungumzia suala hili la Kiswahili. Namshukuru pia Sen. Faki. Ni vile hakutualika pale Mombasa tuweze kusheherekea siku ya Kiswahili duniani. Japo niliona kwa runinga na vyombo vya habari ya kwamba Waziri Aisha Jumwa aliongoza Taifa kwa hicho kikao. Wakati mwingine, naomba tupeleke hayo maadhimisho ya Kiswahili duniani mwaka ujao kwa Seneta wa Embu kwa sababu yeye ndiye ameweka Kiswahili mbele. Ikiwezekana, mwaka unaofuata tupeleke maadhimisho hayo Meru tukizunguka Mlima Kenya, halafu Laikipia ifuate mtawalia. Nashukuru Bw. Spika kwa muda huo wote. Asante."
}