GET /api/v0.1/hansard/entries/1443500/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443500,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443500/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kathuri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13590,
"legal_name": "Murungi Kathuri",
"slug": "murungi-kathuri"
},
"content": "Asante sana Mhe. Spika kwa nafasi hii uliyonipa ili nichangie Hoja iliyoletwa na Kiongozi wa Wengi wakishirikiana na Kiongozi wa Wachache. Kwanza natoa risala za rambirambi kwa wakenya walioathiriwa na vifo 39. Kuna wakenya wengine bado wako hospitali mbalimbali. Nachukua nafasi hii kuwatakia mema na afueni ya haraka. Suala hili limekuja wakati mzuri sana kwa sababu Seneti ni Bunge linalofikiria. Mambo yanapokuwa magumu kwa mataifa, seneti zote duniani ndizo zinakutana ili kurekebisha yale mambo ambayo hayaendi vizuri. Watoto wetu wameongea na sisi tumesikia. Haya mambo hayajaanza jana. Hii Finance Bill tu ni ya kutushtua vile mambo yanavyochemka. Mambo mengi yamekuwa yakiendelea lakini watu hawakuwa wanaongea vizuri. Yale mambo yote ambayo vijana wa Generation Z wameongea, tumeyasikia kama viongozi. Nawaunga mkono kabisa kwa sababu pia mimi niko na kijana aliye katika Kidato cha Tatu. Amekuwa akinieleza mambo mengi kuhusu ufisadi na utumizi mbaya wa rasilimali za umma akiwa likizo. Nilikuwa naona kama anacheza lakini alipofika Kidato cha Tatu, alinieleza kuhusu wizi katika Serikali ama corruption . Nikaona ni kweli amefikiria. Aliniuliza mbona kuna maafisa wa Serikali wanaofanya ufisadi na bado mnawaruhusu kubaki kwa Serikali. Alikuwa anafikiria mahali ninafanya kazi katika Seneti, niko na uwezo wa kusema haya mambo sio mazuri. Aliniambia niko na huo uwezo kwa sababu niko Bungeni. Tena akasisitiza niko na uwezo kwa sababu niko The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}