GET /api/v0.1/hansard/entries/1443501/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443501,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443501/?format=api",
    "text_counter": 90,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kathuri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13590,
        "legal_name": "Murungi Kathuri",
        "slug": "murungi-kathuri"
    },
    "content": "katika uongozi wa Seneti, kwa hiyo niko na nafasi kuu ya kuweza kusaidia Kenya. Nilimwambia alipokuwa kwa likizo ya wiki moja kwamba nimeelewa alichokuwa ananiambia. Bw. Spika, huu ni wakati ambao tunapaswa kukaa chini kama wakenya na tuzungumze vile mambo itaenda. Kuna idara nyingi za serikali ambazo zimetuangusha sana, sana sana shirika la kupigana na ufisadi, EACC. Huwezi kuniambia kesi zote zilizoripotiwa kwa EACC, hakuna hata moja waliyopata ikiwa na wizi ama maofisaa waliofanya makosa. Kama hilo shirika haliwezi kushika hata mtu mmoja miaka hiyo yote wamekuwa, naona badala ya kutumia pesa nyingi katika idara hiyo, afadhali tuongeze bibilia nyingi katika nchi yetu ya Kenya. Pengine kanisa itaweza kuomba. Tumeona mara mbili, wenyekiti wawili, mmoja alikuwa Bishop mkubwa wa kanisa la Anglican Church of Kenya (ACK). Wakati alimaliza muhula wake, tumepewa tena Bishop mwingine lakini sijaona mabadiliko. Naona wakenya lazima waangalie vizuri hilo shirika la EACC. Mhe. Seneta wa Nairobi, mbona sisi tusilete mabadiliko katika mashirika yote ya Serikali kwa sababu sisi ndio wakenya wanaangalia. Sisi tukilia wakati wakenya wanalia pamoja na Generation Z, hakuna kitu tutasaidia wakenya. Ningeomba tushirikiane tukiwa Bunge. Nimefurahi sana kuona pande zote mbili za vyama vya kisiasa zikishishiriana. Huu ndio wakati wa kukaa chini hata kama ni chini ya miti ama kwa shule hapa Nairobi ama university na kuongea tukiwa maseneta wote ndio tuweze kubadilisha nchi yetu. Siku hizi hakuna hata pesa za kuenda Mombasa. Tumeona mambo mengi yaliyoongolewa na vijana hasa kuhusu utumizi mbaya wa pesa za wakenya. Nawashukuru kwa sababu huo ni ukweli. Haswa tukiangalia ugatuzi, saa hizi tumeongeza pesa zikafika Kshs400 billioni. Hizi pesa zote tunapeleka kwa kaunti zetu lakini ni kaunti chache zinazofuata mikataba ya pesa vizuri. Nimeona kaunti zengine wamesema wameongeza ule ushuru walioweza kukusanya ama ownsource revenue . Utakuta Nairobi wameweza kupata Shilingi bilioni kumi. Ukienda Kaunti ya Uasin Gishu, kutoka Shilingi milioni 500, wamefika Shilingi bilioni moja. Kwa hivyo, hizi pesa zote walizokusanya pamoja na ile tutakayowaongezea kutoka Seneti, ni nyingi sana za kusaidika kaunti zetu. Lakini utakuta kwamba magavana wengi--- Ukiangali wengine walivyokuwa mwaka wa 2022 wakiingia kwa kiti, na uwafanyie lifestyle audit ili uone ni mali ngapi wako nayo, utashangaa. Nimesikia mazungumzo kwa mitandao vile magavana wamepata pesa nyingi na kuweza kununua maelfu ya ng’ombe na mashamba mengi. Sasa unashindwa, huu mshahara wa Kshs900,000 ndio umewawezesha kupata mali hii yote kwa muda wa miaka miwili. Kwa hivyo, ni lazima tuchangamke kama wabunge ili tuweze kusaidia Kenya. Bw. Spika, kila wakati tunapoenda kwa uchaguzi, huwa tunaambia wakenya mambo mengi. Je, katika hayo mambo yote tunayowaahidi tutafanya, huwa tunafanya ama tunaongea lakini hatufanyi? Watu wanaoangusha wakenya si Rais bali ni wale anaowapa kazi. Rais wetu wa Kenya yuko na jukumu kubwa la kubadilisha timu yake. Rais ni kama mchezaji na team captain wa mpira wa kandanda. Ukiona mchezaji fulani hawezi kufunga bao, unamuweka kwa bench na kuingiza striker mwengine. Ukiona"
}