GET /api/v0.1/hansard/entries/1443504/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443504,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443504/?format=api",
    "text_counter": 93,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kathuri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13590,
        "legal_name": "Murungi Kathuri",
        "slug": "murungi-kathuri"
    },
    "content": "Idara ingine ninayotaka kumulika ni idara ya usalama. Wakenya wengi wameumia. Siongelei kuhusu zile riots, lakini wakulima wengi wa mifugo wameumia. Tunavyoongea hapa saa hii, kuna bunduki zinalia huko Igembe North kati ya wakaaji wa Samburu wakija kuchukua mifugo ya wameru. Ukijaribu kuongea na mtu yeyote, hakuna mtu anakusikiliza. Security team ya pale Meru hawana uwezo na wale wako Nairobi ni kama hawana uwezo pia. Wakenya wameumia sana haswa katika mpaka wa Meru na Isiolo na Samburu. Tumeumia sana na sijui kama tutaanza kujikinga sisi wenyewe kama Serikali imeshindwa kulinda wakulima na mifugo yetu. Nitaomba Seneti inisaidie katika Jambo hilo. Katika Kaunti ya Laikipia, Mhe. Kinyua kila wakati amewasilisha maombi mengi kuhusu vile ng’ombe wao wanachukuliwa. Sijui kama amepata nafasi ya kufurahia matokeo ya yale aliyojaribu kufanya. Kwa hiyo, nikiwa kama mwakilishi wa Kaunti ya Meru, nitaungana na viongozi wengine wa sehemu hiyo kama Wabunge na viongozi wa Meru County Assembly ndio tuweze kufikiria tutakavyofanya ili tulinde watu wetu na mifugo yetu. Bw. Spika, mambo mengi tunayo ona sasa yanatokana na historical injustices . Watoto wetu wanasema kuwa sisi kama wazazi wao tumefeli katika mambo mengi. Sisi kama viongozi tunawaahidi mambo mengi ambayo hatutekelezi. Kikundi hicho ni cha vijana ambao wamesoma sana na wanaelewa mambo mengi ya kiteknolojia. Mawasiliano yao ni very instant . Wakitaka kuongea wakiwa hata milioni moja, wataingia kwenye mitandao na kuwasilisha ujumbe wao. Mahali tunapoelekea, hata chaguzi zijazo zitakuwa zinafanyika mitandaoni. Kwa hivyo, nasihi wenzangu hapa waishi vizuri na vijana kwa sababu wakiamua kuwa, kwa mfano, hawamtaki Seneta wa Kakamega na waanze kampeni yao kwenye mitandao, siku ya kupiga kura atajipata katika shida. Kwa hivyo, tunyenyekee na kuwasikiliza kwa kufanya mikutano na wao ili tujue mambo ambayo wangependa yafanyike, ili tuishi nao vizuri. Nasisitiza kuwa tujihadhari sana, tuwasikilize na tufuate yale wanayotaka. Kabla kutamatisha, Rais aliteua kamati ya kukagua deni la nchi hii. Alifanya vizuri kwa sababu tangu mwaka 2011 hadi 2021, leo ndio nimeona ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Ripoti hiyo inasema kuwa miradi mingi ya kiwango cha Kshs1.3 trilioni haijulikani ilikoenda. Nafurahi kwa kuwa kamati hiyo iliyoteuliwa itatueleza. Pesa nyingi tunazolipa leo hazikutumika kwa kazi ambazo zilikusudiwa. Huwezi kukopa pesa kulipa mishahara au kufanya mambo mengine. Ukikopa, ni vyema pesa hizo zitumike kwa miradi fulani. Kama hakuna miradi iliyofanywa, tunafaa kuambiwa kazi ambayo pesa hizo zilifanya. Tangu tuwe na “Handshake” katika Serikali iliyopita, mambo yalianza kusambaratika. Ni vizuri tuelezwe bayana kazi iliyofanyika. Bw. Spika, ulinishauri kuwa lazima tufinye mahali ambapo kuna usaha. Tunafaa kushirikiana kama Wakenya kujua shida ilitokea wapi na jinsi ya kutatua. Naomba wanachama wa the Law Society of Kenya (LSK) ambao wamesema kuwa hawataki kushirikishwa katika kamati hiyo wajihusishe. Hata kama Katiba ya Kenya inampa mamlaka Auditor-General kukagua madeni yetu, ni vizuri tuwe na watu wengine wa kutazama. LSK, muungano wa wahandisi pamoja na watu wengine wanafaa wahusike ili tuwe na uhakika kuwa ukaguzi wa deni ulifanywa vizuri. Tunafaa kujua tuna madeni The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}