GET /api/v0.1/hansard/entries/1443510/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443510,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443510/?format=api",
    "text_counter": 99,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, leo Seneti imeamua kuendesha shughuli zake kwa lugha ya Kiswahili. Hivyo basi, kwa heshima kubwa, utaniruhusu pia niendeleze mjadala huu kutumia lugha ya Kiswahili. Asante kwa fursa hii ili kuchangia kuhusu Taarifa hii. Kwa niaba yangu binafsi, familia yangu, na wananchi watukufu kutoka Kaunti ya Kwale, napeana pole kwa familia ambazo zilipoteza vijana wao wakati wa maandamano. Ni huzuni kubwa kuona vijana katika nchi hii wakipoteza maisha kiholela mikononi mwa maafisa wa polisi. Ningependa kutoa ilani kwa the Independent Policing Oversight Authority (IPOA) ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikizembea katika majukumu yake. Hatujawai kusikia kwamba maafisa wa polisi wamepatikana na makosa, kushtakiwa au kuachishwa kazi na hatua kali ya kisheria kuchukuliwa. Kwa niaba ya Gen Z, mara hii hatutakubali IPOA “kutubeba ufala”. Kunradhi Bw. Spika. IPOA inafaa kufanya kazi yake kulingana na sheria. Maafisa wa polisi ambao walitumia nguvu kupita kiasi na kusababisha vijana wetu kupoteza maisha bila hatia yoyote watambuliwe, wachishwe kazi, washtakiwe na hatua ya kisheria ifuate mkondo wake. Mimi nawakilisha vijana katika nchi hii. Nachukua fursa hii kuwapongeza sana"
}