GET /api/v0.1/hansard/entries/1443512/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443512,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443512/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": ". Tumekuwa tukiambiwa kuwa sisi vijana ni viongozi wa siku zijazo. Vijana waliamua kwamba hawatasubiri tena kuwa viongozi wa siku zijazo bali watajihusisha wazi katika siasa na mustakabali wa uongozi wa nchi hii yetu. Nawapa kongole kwa hilo. Tofauti yangu nao ni pale ambapo waliruhusu majangili kuvamia mali, kupora na kuzua ghasia. Hata hivyo, nina imani kuwa tumewasikiliza na kama viongozi, tuko tayari kuketi nao. Kama kiongozi wao, kwa sababu nawakilisha vijana katika Seneti, ninaomba msamaha. Pengine katika upungufu wangu wa kibinadamu, sijaweza kukaa na vijana wenzangu na kusikia kilio chao ili tuweze kukomboa taifa letu na tuwe na nchi ya amani iliyo tayari kusonga mbele. Huu si wakati wa kulimbikiziana lawama kwa sisi kama viongozi. Nimesikia wenzangu wakizungumza hapa lakini sitaki kutaja majina. Walikuwa wanarushiana maneno ambayo haifai kwa viongozi. Ni jambo la kusikitisha kusikia Maseneta wenzangu hapa wakikashifu vikali Wabunge wenzao katika “Nyumba Ndogo” kuhusu"
}