GET /api/v0.1/hansard/entries/1443517/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443517,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443517/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "imependekeza kwamba viongozi au wafanyikazi wa uma wapate nyongeza ya mishahara. Mimi, Sen. Chimera, sina jukumu la kujiongezea mshahara wala kujipunguzia mshahara; kuna tume ambayo inafanya kazi hiyo. Lakini hali ya kiuchumi tuliyo nayo saa hizi hairuhusu kamwe hata kuwe na fikra yoyote ile ya kumuongezea, wacha kiongozi, wacha Mbunge bali hata mfanyi kazi yoyote ule wa uma mshahara. Mimi ninakataa pendekezo lile kama kiongozi binafsi na ninafikiria kuwa sio vyema kwamba tuongezewe mishahara wakati huu, ilhali tunajua nchi ipo mahali pabaya. Tuko na madeni, tunataka kupata ajira kwa vijana wetu. Tunataka kuhakikisha ya kwamba vijana wetu wamepata nafasi sawia ya kufanya biashara na serikali yetu, Vijana wetu wa Gen Z wamelia na wamekuwa na matakwa yao kwa siku nyingi. Kumekuwa na ukandamizaji katika maisha ya vijana wetu. Vijana wetu hawapati fursa ya kufanya biashara na Serikali yetu. Bw. Spika, niruhusu nitihoe ya kwamba hakuna vijana wetu ambao wanapata tenda kwa urahisi. Wanahisi kupata tenda ile ni lazima umfahamu Mhe. Sen. Sifuna kwa mfano, au umfahamu Gavana wa Kaunti ya Kiambu ndiposa uweze kupata tenda. Na wanalilia haki yao. Ni lazima kama viongozi tuaamke, tutengeneze mstakabadhi ambao unampa kijana mkenya fursa ya kufanya biashara na Serikali na kuandikwa kazi katika Serikali bila kumtegemea mtu ambaye anajua au ukipenda, godfather . Ninamshukuru Mheshimiwa Rais William Ruto kwa ile hekima yake ya kuweza kusikia kilio cha vijana wetu na yeye ni kweli ameteremka; ameshuka kutoka pale alipokuwa na yupo tayari kuzungumza na vijana hawa. Ninawaomba hawa vijana wa Gen Z kuwa sisi viongozi wenu tumesikia kilio chenu na tuko tayari kuketi na vijana hawa. Ijapokuwa wanasema kuwa hawana uongozi, nina imani kuwa kutakuwa na muundo ambao tutaweza kuketi kama nchi tuweze kujadiliana, kuridhiana ili tupate fursa ya kusonga mbele tukiwa kitu kimoja, ndiposa nchi hii iweze kuwa na amani, utulivu na tuweze kujivunia matunda ya katiba yetu na nchi yetu ya Kenya izidi kutambulika ulimwenguni kama nchi ambayo ina amani na inamsikiliza mwananchi wake. Kwa hayo mengi, asante, Bw. Spika."
}