GET /api/v0.1/hansard/entries/1443560/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443560,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443560/?format=api",
    "text_counter": 149,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Sheria Endelezi ya Bunge la Seneti katika kuchunguza na kuidhinisha Kanuni za Sheria ya Afya ya Kijamii, zilizoletwa hapa Bungeni na zilizochapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali namba 492004 na 482004. Ningependa kuipongeza Kamati hii ikiongozwa na Sen. Mwenda Gataya Mo Fire kwa umaahiri wake kuchunguza kanuni kama hizi. Kamati ilifanya kazi sana na ikampa Waziri muda wa kutosha kuja kwa Kamati ili kuidhibitishia kwamba alifuata sheria ambazo zinahusika katika kutengeneza sheria kama hizi. Inafaa ieleweke kwamba kwanza, ile haki ya Waziri kutengeneza kanuni kama hizi ni haki ambayo inatolewa na sheria inayopitishwa na Bunge. Tulipopitisha sheria hii, tulikuwa na kikao kule Turkana. Wengi wetu tulikuwa na sababu, tulijua kwamba kuna mambo ambayo Waziri atayaleta na hayo mambo yatasambaratisha ile sheria tulikuwa tumepitisha kwa kauli moja. Imeonekana wazi kutoka kwa hii Ripoti ya Kamati kwamba, Waziri alikosea katika kuchapisha na kuleta kanuni hizi na kwa hivyo, kanuni hizi hazifai kupitishwa na Bunge hili ili ziwe sheria zitakazotumika katika nchi yetu. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia Kamati imesema kwamba, kwanza, hakukuwa na uhusishaji wa umma wa kisawasawa. Kulingana na Katiba, kifungu cha 10 na 118, uhusishaji umma au public participation, ni jambo la msingi ambalo ni lazima lifuatiliwe. Katika kuchunguza mambo haya, kifungu cha 5(a)(1), (d) na (e) cha sheria ya StatutoryInstruments Act, 2013, kinasema ni lazima uhusishaji umma ufanyike na kuwe na ushahidi wa kuonyesha wale waliohusishwa, walioalikwa na wale walituma barua. Kwa hivyo, katika uhusishaji umma, sheria hii haikuweza kufuatiliwa. Katiba ndio mama wa sheria zote katika nchi yetu. Iwapo hawakufuata Katiba, sheria yeyote ambayo inatungwa, itakuwa mbaya. Swala hili la uhusishaji umma tunafaa kuliangazia kwa makini sana kwa sababu juzi, wakati sheria ya Mswada wa Fedha, 2024, ulipopitishwa kule Bunge la Taifa, maoni mengi ya wananchi hayakuzingatiwa. Ndio maana kukawa na migomo na maandamano ambayo hayo mambo yangeondolewa, iwapo ile sheria na maoni ya umma yangefuatwa kutekeleza sheria hiyo. Bw. Spika wa Muda, la kwanza ni kwamba, sheria ya uhusishaji umma haikufuatwa kutengeneza kanuni hizi. La pili kwa kanuni hizi za afya ya jamii, ni kwamba zinahusisha mambo ambayo yangefaa kuwekwa katika sheria kamili. Maswala ambayo yanayotakikana kukaa katika sheria inayopitishwa na Bunge na maswala ambayo yanafaa kukaa katika zile kanuni ambazo Waziri baadaye anaenda kutengeneza kufuatiana na uwezo aliopewa na sheria iliyopita kwa Bunge. Bw. Spika wa Muda, hapa tunazungumzia Kamati ya ushauri ama jopo la ushauri kuhusiana na maswala ya vifurushi vya faida au benefits package pamoja na ushuru unaopaswa kulipwa na kuwekwa katika sheria hiyo. Hili ni jopo ambalo linafaa liwekwa katika ile sheria tunaita sheria mama, yaani parent law, ambayo ni Social HealthInsurance Act . Hiyo pia tunasema kwamba inafanya kanuni hizi kutokuwa sawasawa. Jambo la tatu, katika kifungu cha 31 cha kanuni hizi, kinapingana na sheria ya afya ya jamii kuhusiana na uwezo wa kuamua ni kina nani watakuwa wanatoa huduma kufuatana na sheria hii. Wale ambao wanaita accreditation of health providers . Sheria kuu inasema vingine na kanuni katika kifungu cha 31, inasema vingine. Tunakubaliana The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}