GET /api/v0.1/hansard/entries/1443561/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443561,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443561/?format=api",
    "text_counter": 150,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "iwapo sheria mama, itakinzana na kanuni, basi sheria mama ndiyo huwa inachukua kipau mbele kwa sababu imetungwa na wale waakilishi wa wananchi, moja kwa moja. Bw. Spika wa Muda, jambo la nne ni kuwa Wizara ama jopo husika lililotayarisha maswala haya ama kanuni hizi halikuweza kupambanua maswala fulani yaliyo muhimu katika maswala haya. Kwa mfano, halikuweza kupambanua mfumo wa mchango wa kila mwaka kwa kila familia. Haikuweza pia kuchanganua majukumu ya Serikali kuu na yale ya serikali za kaunti na vile vile, mambo mpito yanayotakikana kuzumgumziwa katika sheria kama hii. Tunapozungumzia mambo mpito ni kwamba, tumetoka katika sheria ya NHIF na tukaenda kwa SHIF. Ni mambo gani wale waliokuwa wakitoa changizo zao katika NHIF watapata katika mfumo mpya? Je, kutakuwa na kupungua kwa mapendekezo au benefits ambazo zinakuja kila mwezi ikiwa mwanachama wa hii SHIF atakuwa mgonjwa? Hayo ni mambo mazito yalifaa kupambanuliwe katika sheria. Bw. Spika wa Muda, jambo lingine ni uhifadhi wa data. Maelezo yangu ninayotoa kulingana na sheria hii yatatumika vipi? Je, yanaweza kutumiwa kuniandikisha mimi kwa chama kingine bali na chama changu cha Orange Democratic Movement (ODM) ama yanaweza kutumika katika mambo sijaruhusu, mimi mwenyewe kama mhusika? Hii ni baadhi ya mambo ambayo tumesema yanafanya kanuni hizi zisipite. Inafaa ieleweke kwamba, katika kuchunguza kanuni hizi, iwapo kutakuwa na jambo moja peke yake ambalo linakinzana na sheria, kwa mfano, ukosefu wa maswala ya uhusishaji umma, ikiwa ni hilo moja, basi linatosha kubatilisha kanuni zote. Kwa sababu, katika sheria hii, hatuna uhuru wa kufanya marekebisho na hatuna uhuru wa kufanya"
}