GET /api/v0.1/hansard/entries/1443563/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443563,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443563/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": ". Kwa hivyo, ni lazima sheria iregeshwe na ichunguzwe tena upya ili iambatane na sheria na zile kanuni zimewekwa kulingana na sheria zilizopitishwa na Bunge hili. Katika Kamati hii ya sheria endelezi, kuna mfumo tunaotumia kwa sasa ambao unampa yule aliyetengeneza kanuni fursa ya kuja mbele ya Kamati kueleza mapendekezo ambayo anataka kuyapeleka. Kamati pia inamshauri vile atakavyofanya ili kuhakikisha kwamba, akileta zile kanuni baada ya kuchapishwa kwa Gazeti Rasmi, haziwezi kukataliwa. Kuna wizara nyingi zilizokubali mfumo huo, lakini masikitiko ni kuwa Waziri wa Afya hakuihusisha kamati kikamilifu katika masuala haya ili iweze kupambanua mambo yanayotakiwa kurekebishwa. Hii ingewezesha kanuni hizi kupitishwa moja kwa moja zifikapo Bungeni. Naunga mkono mapendekezo ya kamati hii kwamba hizi kanuni zibatilishwe kwa sababu kuna mambo mengi yana utata. Kanuni zimesema kwamba manufaa tuliyokuwa tunapata wakati kulikuwa na sheria ya NHIF yamepunguzwa. Haya ni mambo yanayofaa kuangaliwa kwa sababu wananchi wameongeza changizo zao."
}