GET /api/v0.1/hansard/entries/1443599/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443599,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443599/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kama Sen. Cheruiyot, Kiongozi wa Wengi, alivyotangulia kusema, tulipoenda Kitui wakati tulipokuwa katika Kamati ya Sheria ikiongozwa na Sen. Cherarkey, tulizuru Gereza la Kitui tukapata kuwa wananchi wengi wamewekwa rumande kwa makosa madogo ambayo wengine walihitaji Shilingi elfu tatu pekee ili wapate bond waweze kuenda nyumbani na kusubiri kesi zao kusikizwa. Sisi kama Maseneta tuliokuwa pale tulichanga na kuwatoa watu karibu 100 siku hiyo. Nimesahau jina la jaji aliyekuwa anahudumu katika Kaunti ya Kitui lakini alikuwa amehudumu Mombasa pia. Aliweza kupitisha faili zote za wale watu waliokuwa jela na baadaye karibu wafungwa wengine 100 walioweza kutoka jela baada ya hukumu zao kuondolewa na jaji huyo. Kwa hivyo, vikao hivi vina athari nyingi. Kwanza kabisa, inawawezesha Maseneta kuzuru maeneo ambayo sio yao, kuona vile ugatuzi unafanya au haufanyi kazi. Tunapozuru eneo fulani, kila mtu anapata fursa kuangalia mradi mmoja au mwingine kwenye kaunti ambayo tumezuru. Kwa mfano, tulipokuwa Turkana, baadhi yetu tulizuru baadhi ya miradi na wengine kuzuru miradi mingine ambayo ilikuwa imesemekana imefanyika lakini ikawa ni miradi gushi. Vikao hivi vinasaidia pakubwa kuwezesha Seneti kuangalia kama kweli pesa ambazo zinatumwa katika kaunti zetu zinafanya kazi. Bw. Spika wa Muda, pendekezo langu lilikuwa kwamba badala ya kuzuru kaunti moja, Bunge la Seneti ligawanyike kama Kamati 10 za watu sita ambao watazuru kaunti sita tofauti wakati wa hiyo wiki moja ya Seneti mashinani. Ila pendekezo langu lilikataliwa katika Kamati ya Senate Business Committee (SBC). Tutakapozuru Busia, itakuwa bora kwa wale hawakuhusishwa katika Kamiti zao, waweze kuchukua fursa kuangalia ni miradi gani inafanyika ili miradi yote ambayo imeorodheshwa, kwa mfano, Mwaka wa Fedha 2023/2024 iangaliwe ikiwa ilifanyika ua haikufanyika. Mara nyingi pesa zinatolewa kwamba zinafanya miradi fulani lakini ukifika miradi hakuna na pesa zimetumika. Hii inatupa fursa sisi, Maseneta, kutathmini miradi inayofanyika katika kaunti zetu. Vile, inatupa fursa ya kusoma yale mambo yanayofanyika katika kaunti zingine mbali na zetu. Pia, inawapa wananchi fursa ya kusoma majukumu ya Seneti na kazi inayofanywa na Seneti. Kwa hayo mengi na machache, nashukuru kwa kunipa fursa hii."
}