GET /api/v0.1/hansard/entries/1443713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443713,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443713/?format=api",
    "text_counter": 99,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bi. Spika wa muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza nampongeza Waziri kwa taarifa aliyotoa. Niko na swali moja ambalo limegawanyika pande mbili. Je, Serikali inajua kwamba kuna Mkenya anayeitwa Stephen Bertrand Munyakho, Passport No.A353019, ambaye kwa sasa yuko Saudi Arabia na anatajiwa kuuwawa kupitia hukumu ya kifo mnamo tarehe 26 mwezi huu wa saba. Ni jambo gani Serikali ya Kenya inafanya kuhakikisha kwamba maisha ya Mkenya huyo, aliyeshtakiwa kwa makosa ya kuua bila kukusudia yameokolewa na arudi Kenya ajiunge na familia yake pamoja na wakenya wengine? Suali la pili ni kuhusu Mkenya mwengine anayeitwa Nickson Daudi Mwango ambaye alihukumiwa kwa makosa ambayo mahakama haikumpata na hatia ila kwa sasa amewachiliwa lakini yuko katika jela Mjini Riyadh, Saudi Arabia. Anatarajiwa kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kumaliza kesi hiyo. Mwisho---"
}