GET /api/v0.1/hansard/entries/1443751/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443751,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443751/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Kuna dada yetu kwa jina Zuhura Swale Mwabege ambaye alikuwa akifanya kazi Saudia. Aliuawa mwaka jana mwezi wa Disemba. Dada huyu kwao ni Magaoni, Sub-County ya Msambweni. Aliuwawa na mpaka sasa hivi, familia yake haijapata sababu ya kuuwawa kwake Mimi ninakemea sana Embassy yetu ya kule. Sio kwa ubaya lakini tunataka Embassy yetu ya Saudia iamke ifanye kazi. Watu hawa ambao wanafanya kazi kule wanakufa wakiletwa hapa na hakuna sababu tunapewa mtu kuwa amekufa kwa nini ilhali Embassy yetu iko kule kuwakilisha watu wetu. Faida ya kuwa na Embassy kule ni nini? Mpaka sisi viongozi tupige kelele, tupige simu na tuulize ndipo maiti ziletwe. Mimi ninakemea sana Embassy yetu. Na iwapo ninasema uongo, Maseneta wenzangu watasema ukweli. Ni kweli au sio kweli? Wanakufa na hutupati sababu ya kufa kwao. Sasa hivi, ni mwezi wa nne tangu huyo mama afariki. Mpaka leo, familia yake haijajua sababu yake kuuliwa. Maiti ililetwa mwezi wa tatu na tukazika nyumbani. Na sio huyo mmoja pekee, wengi sana wamekufa na sio katika Kwale Kaunti pekee, ni karibu Kenya nzima. Wanakufa huko Saudia na Embassy haipeani sababu ya kifo hicho. Wao ni kimya tu. Tunasema, Embassy iamke na ifanye kazi. Mtu akifa, walete maiti na watuambie amekufa kwa sababu gani. Asante sana, Mheshimiwa Waziri."
}