GET /api/v0.1/hansard/entries/1443794/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443794,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443794/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundingi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Namshukuru Bi. Waziri kwa ile kazi anayofanya ya kubadilisha nchi yetu ya Kenya. Vijana wengi wa Kaunti ya Embu wanapanda miti. Je, watafaidika namna gani na mambo ya carbon credit? Walipanda miti wakati ule mwingine na wakati mlikuwa mnanunua miti, miti yao haikununuliwa. Tuko na ward 20 kule mashinani na subcounty nne na kilio chao ni miti yao haikununuliwa. Vijana wetu watafaidika vipi ili waweze kujisaidia kimaisha wakiendelea kutafuta kazi zingine zinazofaa? Tunajua pia hii inafaa. Pili, nashukuru kwa sababu Kaunti ya Embu ilipatiwa Ksh90 milioni. Nilisikia malalamishi mengi yakitolewa na Gavana kuwa pesa zinaonekana kama nyingi lakini shida ni kwamba pesa nyingi zimetengwa katika kufunza watu mambo mengi. Bi. Waziri, tunaonelea heri mambo ya mafunzo yatengewe pesa kidogo na hizo nyingine ziende kwa kupanda miti. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}