GET /api/v0.1/hansard/entries/1443835/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443835,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443835/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nashukuru Bw. Waziri kwa kuja na kuweka maneno paruwanja kulingana na vile Wizara yake iko, kulingana na mambo ya barabara. Swali langu ni kwamba nimesikia Bw. Waziri akisema ya kwamba alikisia atapata Kshs165 bilioni, lakini akapata Kshs50 bilioni. Kuna zile barabara ambazo zinatengenezwa. Bw. Waziri anachagua vipi barababa itakayotengenezwa na ni ile ambayo haitatengenezwa? Ni maswala gani anaangalia? Ile ilianziwa kitambo ama ile ambayo ina shughuli fulani au ni nini anachoaangazia? Hii ni kwa sababu, nimesikia akisema ya kwamba, Seneta wa Nyamira amekuwa akienda kwake ofisini. Mimi pia, nimeenda kwake ofisini na pia najua Maseneta wengi wamekuwa wakienda ofisini kwake. Pesa ambazo Bw. Waziri ako nazo anasema hazitoshi. Sijui ni mbinu gani anatumia akisema atatengeneza barabara moja katika sehemu ya Laikipia na ile ingine atatengeneza sehemu ya Nyeri. Ni yule ambaye ataenda kwa ofisi ya Bw. Waziri mara nyingi au ni yule atapiga simu mara nyingi ama ni yule Seneta aliye rafiki ya Bw. Waziri? Sijui niseme namna gani lakini ningetaka Bw. Waziri atuelezee na ninashukuru kwa sababu ameweka mambo paruwanja, vile Wakenya wangetaka ili wajue ya kwamba unatumia zile pesa unazo vipi."
}