GET /api/v0.1/hansard/entries/1444144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1444144,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1444144/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu kuhusu wachuuzi wa rejareja. Kwanza, nampongeza Sen. Esther Okenyuri kwa Mswada huu. Amewapa heshima na hadhi wachuuzi ambao kwa wakati mwingi wanaonekana kama watu wasiofaa ama biashara wanazofanya hazifai. Kwa kuwasilisha Mswada huu hapa Seneti, inaonyesha kwamba anawajali. Ukitazama Vifungu vya tatu na nne, Waziri anayehusika atapaswa kujua idadi ya wachuuzi katika Jamhuri ya Kenya. Baada ya kujua idadi, itamwezesha kuleta usawa katika sehemu zinazofanyiwa kazi; iwe kule Nyahururu, Nanyuki, au Nyaribari Chache. Wachuuzi wote wanapaswa kufanya uchuuzi katika mazingira sawa. Sio mara moja tumewapata wachuuzi wetu wakiishi kwa maisha ya kukimbizwa kila mahali. Ukienda Nyahururu, utapata wanafukuzwa mchana kutwa kutoka sehemu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}